Soko la Big Brother Manzese Dar lavunjwa

Kwa waliowahi kufika Dar es Salaam wanaweza kuwa wanalifahamu soko maarufu la mitumba linaloitwa kwa jina maarufu la Big Brother limevunjwa na sasa wafanyabiashara takribani elfu tatu waliokuwa wakiendesha biashara eneo hilo wanahaha kutafuta eneo lingine. Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia, FFU walilazimika kuwatawanya wafanyabiashara hao kwa mabomu na risasi hewani walipotaka kufunga barabara siku moja baada ya maeneo …

WAZIRI MKUU ASHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO MKOANI KAGERA LEO.

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Zamzam kwenye Manispaa ya Bukoba akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera leo. Kushoto ni mkewe Tunu na kulia kwake ni mkuu wa mkoa huo, Mohamed Babu. Picha ya Juu: Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa amevaa kofia aliyozawadiwa na wananchi wa Manispaa ya Bukoba baada ya …

JK ataka bil 54 zilizotoweka kwenye madini zisakwe

Na Mwandishi Maalumu Paris, Ufaransa RAIS Jakaya Kikwete amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kuchunguza kiasi cha sh. bilioni 54 ambacho kimebainika kimepotea kutoka katika malipo ya tozo na kodi mbalimbali katika sekta ya madini. Kikwete ametoa maagizo hayo jana mjini hapa alipokuwa akihutubia wajumbe katika Mkutano wa Tano wa Mpango wa Uhamasishaji wa …

Wabunge wa Tanzania wanajipendelea-DOVUTWA

Na Mafikiri Ernest Dar es Salaam CHAMA cha UPDP kimehoji uhalali wa kila mbunge kulipwa Sh 90 milioni kama mkopo kuwawezesha kununua magari binafsi ya shughuli za kibunge huku wafanyakazi wa kada nyingine za kitaalamu zaidi wakisahaulika katika mpango kama huo. Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, Mwenyekiti wa taifa wa UPDP Fahmi Nassoro Dovutwa amesema uamuzi …

JE ALIYELALA AAMSHWE?

Huyu si mwingine bali ni waziri mwenye dhamana ya kuiongoza wizara ya nishati madini mheshimiwa sana bwana William Ngeleje, waziri ambaye wizara yake imekuwa ikilalamikiwa kwa ufisadi na utata katika mikataba feki , pembeni kabisa mwa bosi wake na mkuu wa nchi, tena kwenye mkutano wa kimataifa, jionee mwenyewe jinsi anavyouchapa usingizi bila hata kuwa na shaka na wasi, kwa …

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOMAINDO-MASASI.

Watendaji wakuu wa halmashauri za wilaya wametakiwa kushirikiana ili kuboresha na kuimarisha huduma za afya nchini. Wito huo umetolewa jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda alipofanya ziara ya kikazi katika wilaya ya masasi. Dkt. Mponda alisema ili huduma za afya ziimarike ni vyema watendaji hao kushirikiana kwa pamoja na bodi ya afya za halmashauri …