08 March 2011 Arusha WATU wanaodaiwa kuwa ni vigogo wa Serikali wamesababisha vurugu kubwa katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo kunakotolewa tiba ya magonjwa ya sugu na Mchungaji Mstaafu, Ambilikile Mwasapile baada ya kuvuruga utaratibu wa foleni kabla ya kupata huduma hiyo. Vurugu hizo zilianza pale kundi la watu lilipobaini kuwa vyombo vya dola, askari polisi na wanamgambo …
Tanesco wadaiwa tena mamilioni Kenya
Na Mwandishi Wetu Namanga LICHA ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) kutakiwa kulipa deni la sh. bilioni 94 kwa kampuni ya Dowans ambazo bado zimeleta utata, imebainika kuwa shirika hilo pia linadaiwa sh. milioni 175 na Shirika la Umeme nchini Kenya (KPLC). Shirika hilo la kusambaza umeme Kenya, limekuwa likitoa huduma ya umeme katika baadhi ya maeneo yaliyo …
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein otembelea mashamba ya kilimo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akipewa maelezo kutoka kwa Ofisa Mdhamini Pemba wa Wizara ya Kilimo na Mifugo, Dk Suleiman Sheikh Mohamed, wakati alipotembelea mashamba ya kilimo huko, Bonde la Kwajibwa, Kengeja, Kusini Pemba, kuangalia athari za kiangazi zilizowakumba wananchi wa maeneo hayo, watatu kushoto ni mkewe Mama Mwanamwema Shein.
MH. KOMBA AMETUMWA BUNGENI AKALALE?
Kwa mpango huu ndugu zangu tutafika? Baadhi ya waheshimiwa wetu wamekuwa ni watu wa kuhudhuria vikao tu, na mara nyingi huwa wanalala wakati vikao vya kujadili maslahi ya nchi vikiendelea. Hilo pozi la Mh. John Komba, ambaye ni mbunge wa Mbinga Magharibi linaonyesha kabisa kwamba amejiweka “comfortable” ili aweze kupata kauisingizi kidogo.
Mwananchi alipukiwa na bomu Lindi
Na Mwandishi Wetu Lindi MKAZI mmoja wa kijiji cha Kitumbikwera mkoani Lindi, Omari Said (29) amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine akiuguza majeraha aliyoyapata baada ya kulipukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu. Tukio hilo limetokea hivi karibuni mjini hapa na majeruhi amelazwa wodi namba sita ambapo ameumia vibaya sehemu ya mgongoni, ubavuni, matakoni pamoja na kukatika kiganja cha …
Wanne wapandishwa kizimbani kwa dawa za kulevya
Na Mwandishi Wetu RAIA wanne wa mataifa tofauti, jana wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kosa la kula njama na kuingiza dawa za kulevya nchini zenye thamani ya sh bilioni 2.8. washtakiwa hao ambao ni Dennis Okechukwa, Paul Obi ambao ni raia wa Nigeria, mwingine ni raia wa Afrika Kusini, Stani Hycenth pamoja na raia wa nchini …