Askari waliogombea mirungi wasubiri hukumu

      Na Mwandishi Wetu, Mwanza ASKARI polisi wawili wanaodaiwa kupigana baada ya kushindwa kugawana dawa za kulevya aina ya mirungi iliyotelekezwa na abiria mmoja hivi karibuni mjini hapa wameshitakiwa kijeshi na Jeshi la Polisi na sasa wanasubiri kuhukumiwa. Akizungumza na Jmwandishi jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Simon Sirro amesema askari hao tayari wameshtakiwa kijeshi na …

Dk Shein: Tumuenzi Karume kwa vitendo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka vijana kumkumbuka Marehemu Abeid Amani Karume kwa vitendo. Dk. Shein aliyasema hayo janna baada ya kupokea matembezi ya kumuenzi muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar marehemu, Abeid Karume katika viwanja vya Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui, mjini Zanzibar. Matembezi hayo ambayo yamefanywa …

TUNDU LISSU MATATANI

    SPIKA Anne Makinda, amempa siku mbili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kuthibitisha kauli yake aliyoitoa bungeni jana kwamba Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ni mwongo. Alisema mbali na Lissu kuthibitisha kauli yake, yeye (Spika) atatoa taarifa juu ya Mbunge wa Arusha, Godbless Lema (Chadema), ambaye kwenye Mkutano uliopita alitaka kujua hatua zinazochukuliwa kwa kiongozi …

Babu Loliondo afanya maajabu

Na Mwandishi Wetu, Loliondo MIUJIZA ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile wa Kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro juzi Ilijidhihirisha kijijini hapa baada ya mmoja wa wezi aliyechomoa pochi ya mgonjwa raia wa Kenya kusalimisha pochi hiyo kwa Mchungaji huku akidai anapigwa na watu asiowaona na kushindwa kuona. Aprili 2, 2011 mmoja wa raia kutoka nchini Kenya aliibiwa pochi iliyokuwa na fedha …

Usiyoyafahamu kuhusu Mchungaji Mwasapila

  HIVI unafahamu kwamba Mchungaji Ambilikile Mwasapila ambaye umaarufu wake umepanda kwa kasi kutokana na kutoa tiba ya magonjwa sugu, ni yatima ambaye hakuwahi kuwafahamu baba na mama yake? Mwasapila ambaye ni Mchungaji Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), anasema hakuwahi kuwatambua wazazi wake kwani walifariki dunia akiwa na umri mdogo hivyo kulelewa na wajomba zake.

Majaji 12 wapata kikombe kwa Babu

MAJAJI 12 ambao ni wakuu wa Kanda za Mahakama Kuu ya Tanzania, jana waliingia katika orodha ya vigogo kufika Samunge, Loliondo kupata tiba ya magonjwa sugu kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila. Habari zilizopatikana jana zimeeleza kwamba majaji hao walifika Samunge wakitokea Arusha ambako walikuwa na semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Idara ya Mahakama katika kushughulikia kesi za ukiukwaji wa haki …