Chadema wachoma moto muswada wa marekebisho ya Katiba

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Hamad Mussa Yussuf , akichoma moto mswada wa sheria ya kuanzisha Tume ya kurekebisha Katiba Tanzania leo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar. Picha na Hamad Hija,MAELEZO Zanzibar

YANGA BINGWA TANZANIA, SIMBA MAMBO MABAYA

BAADA ya timu ya Yanga ya Dar es Salaam kutangazwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, hali imekuwa mbaya kwa wapinzani wao wa jadi timu ya Simba na sasa wameanza kutimuana. Yanga na Simba wameringana pointi yaani wote wamefikisha pointi 46 kila mmoja ila Simba amefungwa magoli 17 huku Yanga akifungwa magoli 7 tu, sehemu ambapo amemzidi mpinzani …

Jiwe lauwa mchimba madini Bulyanhulu

Na Mwandishi Wetu Kahama MFANYAKAZI mmoja katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga amefariki dunia baada ya kuangukiwa na jiwe wakati akilipua miamba ya dhahabu mgodini. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bahati Matala alisema mfanyakazi huyo alifariki dunia usiku Aprili 9 mwaka huu baada ya kuangukiwa na …

Walimu 81 wakacha kuripoti Rukwa

Na Mwandishi Wetu Sumbawanga ZAIDI ya walimu 81 waliopangiwa kufundisha shule mbalimbali za sekondari zilizopo mkoani Rukwa hawajaripoti katika vituo vyao vya kazi, limefahamika. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana mjini hapa Ofisa Elimu, Taaluma Mkoa wa Rukwa, Albert Mloka alisema walimu hao ni kati ya walimu 303 waliopangiwa na Serikali mwezi Januari mwaka huu kufuatia mkoa huo kuwa …

Mkama, Kinana watajwa kubeba jahazi la CCM

Dodoma SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu pamoja na sekretarieti yake, baadhi ya makada wa chama hicho tawala wanatajwa kujaza nafasi za utendaji. Taarifa kutoka ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu jana usiku mjini hapa zilidai kuwa Wilson Mkama ndiye aliyepewa jukumu la Ukatibu Mkuu wa CCM huku msaidizi wake kwa upande wa Bara …

Viongozi wa siasa wafanyabiashara maarufu kutekwa

Na Mwandishi Wetu MNAJIMU maarufu nchini, Sheikh Yahya Hussein ametabiri kuwa viongozi wa siasa na wafanyabiashara maarufu watatekwa kuanzia Aprili 19 na kuendelea hadi mwezi Julai. Utabiri huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na mnajimu huyo na kusambazwa katika vyombo vya habari. Hata hivyo hakuweka wazi kuwa ni viongozi gain watatekwa au kutaja watu au makundi ambayo yatawateka. “Viongozi …