Dewji amwaga mahindi tani 100 kwa wapigakura wake

Na Mwandishi Wetu Singida MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Dewji, ametoa msaada wa tani 100 za mahindi zenye thamani ya sh. milioni 40 kwa wananchi wa vijiji 20, wanaokabiliwa na upungufu wa chakula kwenye jimbo hilo. Akizungumza jana katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo, Dewji alisema amefikia uamuzi huo wa …

DC Serengeti akemea matapeli wa safari za Loliondo

Na Mwandishi Wetu Serengeti SERIKALI wilayani Serengeti mkoani Mara, imekilalamikia kitendo cha baadhi ya wafanyabiashara kuendelea kutumia malori kusafirisha wagonjwa kwenda Loliondo kupata tiba kwa ‘Babu”, kwani kimekuwa kikileta usumbufu baada ya wagonjwa kuzuiwa na vyombo vya dora. Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Edward ole Lenga, alisema kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakipakia watu kwenye malori na kupita njia za panya …

Diwani Chadema amshtaki Mkurugenzi wa Halmashauri

Na Mwandishi Wetu Sumbawanga DIWANI wa Kata ya Makanyagio wa Chama cha Demikrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilayani Mpanda, Iddy Nziguye amemfikisha mahakamani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda, kwa tuhuma za kutumia sheria za halmashauri ya mji huo kabla hazijapitishwa na kuthibitishwa kitaratibu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana mjini hapa na Diwani Nziguye amethibitisha kuwa amefungua kesi hiyo …

Kilimo Kwanza bado akijamnufaisha mkulima

Na Mwandishi Wetu Morogoro DHANA ya Kilimo Kwanza imeshindwa kuwanufaisha wazalishaji wadogo wadogo wanaoishi vijijini kutokana na rasilimali zinazotakiwa kuelekezwa katika maeneo hayo kushindwa kutolewa kwa wakati, tafiti zimebainisha. Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Ardhi, Yefred Myenzi, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye warsha ya changamoto za Kilimo Kwanza kwa wazalishaji wadogo kutoka …

WILSON MUKAMA, NEW CCM SECRETARY GENERAL!

CCM has picked retired longserving civil servant and party cadre Wilson Mukama as its new Secretary General, replacing Mr Yussuf Makamba who resigned alongside other members of the party’s Central Committee (CC) and entire secretariat on Saturday night.

Wilson Mukama awa Katibu Mkuu CCM

HATIMAYE kitendawili cha mageuzi mkubwa ya CCM kupata viongopzi wapya wa Kamati Kuu (CC) ya Chama hicho kimeteguliwa na sasa atakayeshika nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa ni Wilson Mukama, huku akisaidiwa na John Chiligati kama Katibu Msaidizi aliyekuwa mwenyekiti Itikadi na Uenezi wa uongozi uliojiuzulu. Viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na Nape Mnauye, anaye kuwa Katibu wa …