Babu wa Loliondo awashukia wanaomuiga

Ngorongoro MCHUNGAJI mstaafu Ambilikile Mwasapila (Babu) amesema baadhi ya watu wanaodai kutibu kwa kutumia tiba ya kikombe kama anavyofanya yeye ni wauaji, wezi na wanasumbuliwa na njaa, hivyo amewataka wananchi wawapuuze. Akizungumza na waandishi wa habari kutoka Jijini Mwanza, Aprili 13 mwaka huu, Mwasapile alisema watu walioibuka baada ya yeye kuanza kutoa huduma ya tiba ya kikombe wanasumbuliwa na njaa …

Bunda wata ushuru wa magari ya Loliondo

Bunda HALMASHAURI ya Wilaya ya Bunda, inatarajia kufanya mazungumzo na uongozi wa wilaya hiyo, ili iruhusiwe kukusanya ushuru kwenye magari yanayofika katika kituo cha Bunda, kwa ajili ya kupeleka watu kwa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, Loliondo Arusha, kupata tiba ya mchungaji huyo. Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na madiwani wa halmashauri hiyo, wakiongozwa na Mwenyekiti, Joseph Malimbe, kwenye kikao …

Akamatwa akimiliki duma kinyume cha sheria

Na Mwandishi Wetu Arusha KIKOSI cha Kupambana na Ujangili Kanda ya Kaskazini kinamshikilia Rahman Hassan kwa tuhuma za kupatikana na wanyama aina ya duma (Cheater), huku watatu akiwa amewaficha nyumbani kwake eneo la Sombetini Arusha. Duma hao inadaiwa wamekamatwa na badhi ya wafanyabiashara maarufu katika Jiji la Arusha na inasadikiwa walikuwa wanasafirishwa kwenda nje ya nchi. Kaimu Kamanda wa Kikosi …

Butiku: Serikali iwe sikivu mjadala Katiba mpya

MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku ameitaka Serikali kuwa sikivu na kusikiliza wananchi wanataka nini juu ya mchakato wa katiba mpya na si wanasiasa na viongozi wa juu kujiamulia watakavyo. Butiku ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika Kongamano la miaka mitatu ya Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere lililomalizika jana Chuo Kikuu cha Dar …

Basi la Ngorika laua tisa na kujeruhi 16

Na Mwandishi Wetu Arusha WATU 9 wamefariki dunia na wengine nane kujeruhiwa huku wanne kati yao wakiwa na hali mbaya, baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana na kupinduka katika eneo la Makumira wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye, alisema kuwa tukio hilo limetokea leo majira ya saa 12:30 asubuhi nje kidogo …

Takukuru ‘yawalinda’ wezi wa mifugo Karagwe

    Na Mwandishi Wetu Karagwe WANANCHI mkoani Kagera wanaituhumu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa inajihusisha na vitendo vya kuwalinda wezi wa mifugo kutoka nchi jirani kinyume cha sheria huku wakiweka mbele maslahi yao. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyopatikana wilayani Karagwe hivi karibuni vimemtaja Ofisa wa mmoja wa TAKUKURU (jina tunalo) kuwa amekuwa akiwalinda …