Mwalimu acharaza viboko 100 wanafunzi

WAKATI Serikali ikijaribu kupunguza adhabu za viboko kwa wanafunzi na kuweka mwongozo na utaratibu wa adhabu hizo, wananfunzi wanne wa Shule ya Sekondari Nsoho mkoani Mbeya wamejeruhiwa baada ya kuchapwa viboko 100 kila mmoja. Tukio hilo linadaiwa kufanywa April 22 mwaka huu na mwalimu Lukindo Mwakanyasi,ambaye anafundisha shuleni hapo kwa mkataba. Wakizungumza hivi karibuni kwa masharti ya kutotajwa majina, baadhi …

JK amteua Mshana kushika nafasi ya Tido TBC

RAIS JAKAYA KIKWETE JANA ALIMTEUA ALIEKUWA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI-MAELEZO, CLEMENT MSHANA KUWA MKURUGENZI MPYA WA SHIRIKA LA HABARI TANZANIA (TBC) KUZIBA NAFASI ILIYOACHWA WAZI NA MKURUGENZI ALIEMALIZA MUDA WAKE, TIDO MHANDO.UTEUZI HUO UMEFANYWA LEO NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE.

Katibu wa Bunge awaponda wabunge

Na Mwandishi Wetu KATIBU wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Thomas Kashililah amesema wabunge wengi kutofahamu vema kanuni za uendeshaji wa Bunge, ndiyo chanzo cha mivutano na vijembe kutawala vikao vya Bunge la 10. Kashililah alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hali hiyo pia inachangiwa na uwepo wa …

Dk Shein kutembelea Uturuki

Na Rajab Mkasaba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuondoka nchini Aprili 28 kuelekea Jamhuri ya Uturuki kwa ziara ya mwaliko wa rais wa nchi hiyo, Abdullah Gul. Katika ziara hiyo, Dk. Shein atafuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Waziri wa Nchi Ofisi ya …

Irani yatoa USD mil 1.2 kusaidia Kilimo Kwanza

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Irani imepanga kutoa dola za kimarekani milioni 1.2 (dola milioni 1.2) kuisaidia Tanzania katika utekelezaji wa vitendo kampeni za Kilimo Kwanza. Taarifa imetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati Balozi Msaidizi wa Iran nchini Tanzania Bahman Ahmadi alipotembelea Wizara ya Viwanda na Biashara na kuzungumza na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Lazaro Nyalandu. Katika mazungumzo …