Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam Taarifa zilizotufikia asubuhi hii ni kwamba madereva wa mabasi ya kutoka Dar es Salaam kuelekea mikoani wamegoma kufanya safari zao na hadi sasa hakuna basi lolote lililoondoka kutoka kituo kikuu cha mabasi hayo cha Ubungo. Kwa mujibu wa abiria mmoja ambaye ni msafiri ameiarifa dev.kisakuzi.com kuwa miongoni mwa mambo ambayo madereva hao wanadai ni …
RUBADA yawekeza katika umeme
MAMLAKA ya Uendeshaji wa Bonde la Mto wa Rufiji (RUBADA) jana ilitia saini mkataba wa uzalishaji wa umeme na Kampuni ya Sinohydro ya nchini China kwa ajili ya kuzalisha umeme katika eneo la Mpanga, lililopo ndani ya Bonde la Kilombero. Akizungumza katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa RUBADA, Aloyce Masanja, alisema mradi huo utaanza hivi …
Vijiji 150 vyakumbwa na njaa Nzega
Na Mwandishi Wetu Nzega WAKAZI wa wilaya ya Nzega pamoja na vitongoji vyake vimekumbwa na gharika kubwa la njaa, baada ya mvua za masika kutonyesha kikawaida. Kutokana na hali hiyo sehemu mbalimbali za wilayani hapa zimekumbwa na ukame uliyosababisha njaa kwa wakazi wa vijiji anuai. Wilaya ya Nzega ndiyo iliyoathirika zaidi kwani takribani vijiji 150 vimekumbwa na njaa na sasa …
Shule za Serikali zapeta Kidato cha Sita
SHULE za Sekondari za Serikali zimeng’ara katika matokeo ya Kidato cha sita mwaka 2011 baada ya wanafunzi wake saba kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora kitaifa.Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa jana jijini Dar es Salaam, wanafunzi kumi waliofanya vizuri zaidi kitaifa ni wavulana.Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako aliwataja wanafunzi …
Dk Shein awasili nchini Uturuki kwa ziara
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania, Dk. Sander Gurbuz, (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Ankara nchini Uturuki, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika ziara rasmi kufuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo.
Tamasha la Vodacom ‘Shuffle Dance’ Dar
Wasanii mbalimbali na vijana waliojitokeza kushiriki Tamasha la Vodacom ‘Shuffle Dance’, wakicheza staili moja kwa pamoja wakati wa Tamasha hilo lililofanyika juzi kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Sunrise Kigamboni Dar es Salaam, Tamasha hilo likiwa na lengo la kuvunja na kuweka rekodi ya Dunia katika kitabu cha Matukio Makubwa yanayotokea duniani, ‘Guinness Book Records’. Tamasha liliandaliwa na kampuni ya simu …