‘Siasa zisiingizwe kwenye shughuli za maendeleo’

Na Anna Nkinda, Maelezo Mkuranga WANANCHI wilayani Mkuranga wametakiwa kuachana na itikadi za kisiasa katika shughuli za maendeleo, kwani suala la maendeleo linamgusa kila mwananchi bila kujali itikadi za kisiasa. Wito huo umetolewa jana mjini hapa na mke wa Rais, Salma Kikwete wakati akifungua Chama Cha kuweka Akiba na Kukopa (SACCOS) kitakachojulikana kama ‘Salma Kikwete’ kilichopo kijiji cha Hoyoyo Mkoa …

KIFO CHA OSAMA:NDIO HATMA YA DONALD TRUMP KISIASA?

Nilipokiona hichi kikaragosi cha ndugu yetu GADO, niliguswa sana na nikaona sina budi kuandika mawili matatu hapa katika baraza letu la uchambuzi nyeti.  Tajiri la vitega uchumi wa majumba Marekani, Bw. Donald Trump ameumbuka hivi karibuni kutokana na ile hulka yake ya kudadisi na kutilia mashaka uraia wa Rais Obama. Siku za hivi karibuni, Trump amekuwa mstari wa mbele kuwahimiza …

JK: Kifo cha Osama ni unafuu kwa walioumizwa

Na Edson Kamukara Dar es Salaam RAIS Jakaya Kikwete amesema kifo cha Kiongozi wa kundi la Al-qaeda, Osama Bin Laden kitaleta unafuu na kuwapunguzia machungu watu waliopoteza ndugu zao ama kujeruhiwa katika matukio yaliofanywa na kundi hilo wakiwemo Watanzania. Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kwenye mkutano wa Tume ya Shirika la Umoja …

Mmethibitisha Obama ni Mmarekani si Mwafrika

WAKATI Barack Hussein Obama alipotangazwa kama mshindi anayengoja kuapishwa na kuwa Rais wa 44 wa Marekani, niliandika makala, ‘Obama ni Rais wa Marekani si Rais wa Afrika.’ Niliandika hivyo kwa makusudi kutokana na matumaini makubwa, na pengine yanayozidi kawaida walivyokuwa nayo baadhi ya Waafrika kutokana na rangi ya Obama. Nchi jirani ya Kenya (alikotoka Hussein Obama) ilitangaza siku moja rasmi …

Ubungo yachafuka

*Madereva wa mabasi ya mikoani wagoma *Abiria wataabika, FFU watembeza virungu *Kova azomewa, aambiwa aache siasa VURUGU kubwa za aina yake, ziliibuka jana katika Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani kilichopo Ubungo Dar es Salaam, baada ya madereva wa mabasi kugoma wakilalamikia mikataba ya ajira. Sambamba na malalamiko hayo, wadereva hao waligoma kwa sababu hawaridhishwi na utendaji kazi wa Kikosi …

Abiria wa safari za mikoani wasota Ubungo

Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mai Mosi) Dar es Salaam yameingia dosari baada ya madereva wa mabasi yaendayo mikoani kugoma kwa saa nane kabla ya kuendelea na safari zao, hali iliyozua kero kubwa kwa abiria waliokuwa wakielekea sehemu anuai mikoani na nje ya nchi. Madereva hao jana katika Kituo Kikuu cha Mabasi ya …