CALIFORNIA, Marekani MWISHO wa dunia umefika na huenda tusiione tena Jumapili ya kesho kwani dunia inafikia mwisho wake leo Jumamosi, kwa mujibu wa Mchungaji wa Kanisa moja la California. Mchungaji Harold Camping wa California, ametabiri kuwa mwisho wa dunia ni leo Mei 21 mwaka huu saa moja kamili usiku. Mchungaji Camping kwa kutumia mahesabu ya tarehe na mafunzo ya Biblia, …
Mbunge Nyangwine afichua ‘siri’ vurugu za Tarime
Na Joachim Mushi MBUNGE wa Tarime kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nyambari Nyangwine amesema walioshambulia msafara wake hivi karibuni wilayani Tarime ni kundi la watu lililoandaliwa na baadhi ya madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, ambao hawakupenda jimbo hilo kuchukuliwa na CCM. Nyangwine pia amepinga taarifa zilizotolewa kuwa alishambuliwa na wananchi na kujeruhiwa kisha kulazwa hospitalini, na …
Mauaji Tarime; LHRC wataka mgodi wa Barrick ufungwe
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) kimeitaka Serikali kufunga uzalishaji katika mgodi wa Barrick hadi hapo ufumbuzi wa kudumu utakapopatikana juu ya mgogoro uliopo. Akizungumza jana Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Francis Kiwanga aliishauri Serikali ifanye hivyo kutokana na mauaji yaliyofanywa na polisi katika mgodi huo uliopo Nyamongo wilayani Tarime. Alisema LHRC inalaani vikali mauaji …
Mauaji raia Tarime, Polisi waelemewa
Na Joachim Mushi JESHI la Polisi nchini limekata tamaa kuendelea na juhudi za kuwashawishi ndungu wa marehemu wa miili iliyouwawa kwa risasi baada ya kundi la watu takriban 800 kudaiwa kuvamia mgodi wa Barrick na kutaka kuiba mchanga wa madini mgodini hapo. Akizungumza kwa njia ya simu jana kutokea Tarime, Kamishna Oparesheni wa Polisi, Paul Chagonja alisema wameamua kuwaachia ndugu …
M/Kiti Halmashauri Rungwe auwawa kwa risasi
Na Dotto Mwaibale Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya (CCM), ambaye ni diwani wa Kata ya Kiwira, John Mwankenja, ameuawa kwa kupigwa risasi tatu kichwani na watu wasiojulikana. Tukio hilo ambalo limewasikitisha watu wengi waliokuwa wakimfahamu marehemu limetokea juzi saa tatu usiku muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwake akitokea mkoani Mbeya kumuona mkewe Lyidia Mwakatumbula ambaye …
Dowans yauzwa kwa Wamarekani
Na Joachim Mushi HATIMAYE kampuni ya kuzalisha umeme ya Symbion ya nchini Marekani imetamka rasmi kuwa tayari imenunua mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans iliyopo eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Meneja Mtendaji wa Symbion, Paul Hinks (pichani juu akiwa na Mwenyekiti wa Symbion, Balozi mstaafu Joseph …