Na Mwandishi Wetu Tarime MBUNGE wa Jimbo la Singida Kusini kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na wezake saba jana waliachiwa baada ya kupata dhamana ya masharti matatu likiwemo la kusaini hati zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 70. Mbali na Lissu watuhumiwa wengine waliofikishwa juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime kwa kesi no. 210 ya mwaka 2011 ni mkurugenzi …
Hali si shwari CCM Arusha
Hili ni tamko la baadhi ya wajumbe wa UVCCM Arusha Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumeona tuwaite hapa ili tuweze kutoa maoni yetu kuhusiana na mustakabali wa chama chetu cha Mapinduzi na Jumuiya yetu ya Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha. Tumewaita hapa kwa malengo makuu Sita:- Kuunga mkono Halimashauri kuu ya CCM Taifa kwa kuona umuhimu …
TGNP WATOA MUONGOZO WA BAJETI 2011/16
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) kupitia kikundi kazi chake cha uchambuzi wa bajeti (Budget Analysis Task Team) wakishirikiana na wanaharakati wengine kutoka ngazi ya jamii wamefanya uchambuzi wa muongozo wa mpango wa miaka mitano wa bajeti kwa mwaka wa fedha utakaoanza Julai mwaka 2011/2012 hadi 2015/16 . Uchambuzi huu umefanywa kwa mtazamo wa ukombozi wa wanawake kimapinduzi, wakiongozwa na kauli …
Naibu Waziri wa Afya ataka waganga wakamatwe
Na Mwandishi Wetu Morogoro NAIBU Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kuwachukulia hatua za kisheria watu waganga wanaobandika mabango kujitangaza wanatibu magonjwa sugu kumbe wanafanya utapeli. Dk. Nkya alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati wa semina ya Ukimwi kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na watendaji wa …
JK amteua Mkaguzi Mkuu ndani ya Serikali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete amemteua Bw. Mohammed A. Mtonga (52) kuwa Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Serikali. Bw. Mtonga ni msomi mwenye Shahada ya Uzamili katika masuala ya Fedha (MSc in Corporate Finance) toka Chuo Kikuu cha Salford nchini uingereza. Aidha Bw. Mtonga anayo Shahada ya Uhasibu ya CPA (T) inayotolewa na Bodi …
Ajali; Wawili wafa 28 wajeruhiwa Iringa
Francis Godwin Iringa WATU wawili wamekufa papo hapo na wengine 28 kujeruhiwa vibaya baada ya fuso lenye namba za usajili T115 ANZ walilokuwa wakisafiria kwenda Mnadani Pawaga Iringa kupinduka. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 1 asubuhi leo katika Milima ya umasaini barabara kuu ya Iringa -Pawaga wakati wafanyabiashara hao zaidi ya 50 wakielekea mnadani huku chanzo cha ajali hiyo …