Na Janeth Mushi, Arusha HAKIMU mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Charles Magesa amemuamuru Ofisa wa Kituo Cha Polisi mkoani hapa kutekeleza amri ya Mahakama ya kumkamata Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe kwa kushindwa kutii amri ya Mahakama. Hakimu Magesa ametoa agizo hilo leo mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi …
Wasichana wakamatwa wapimwa bikra Misri
Shirika la kutetea haki za binaadam la Amnesty International limeitaka serikali ya Misri kufanya uchunguzi kamili baada ya maofisa wa juu wa kijeshi kukiri kuwa waliwafanyia vipimo vya ubikira, wanawake waliokuwa wakiandamana hivi karibuni. Pamoja na hayo, Amnesty imetaka wote waliohusika kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu udhalilishaji huo. Tuhuma hizo ambazo zinadaiwa kutokea kwa wanawake waliokuwa wakiandamana baada …
Oxfam yaja na kampeni mpya ya ‘otesha’
OTESHA ni kampeni mpya ya Oxfam ya juu ya njia bora za kuotesha, kugawana na kuishi pamoja. Ni kampeni yetu sote, mabilioni ya watu tunaokula chakula na zaidi ya wenzetu bilioni moja wanawake na wanaume wanaozalisha chakula hicho. Ni kampeni yenye kutafuta suluhisho kwa mustakabali bora wenye uhakika wa chakula kwa kila binadamu. Hivi karibuni idadi ya watu itafikia bilioni …
Mgogoro UVCCM Arusha, wenyeviti wilaya watoa tamko
Na Janeth Mushi, Arusha IKIWA zimepita siku chache tangu makundi mawili ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha kufanya maandamano yaliyokuwa na madai mbalimbali, wenyeviti wa umoja huo kutoka wilaya zote sita mkoani Arusha wamekutana na kutoa kauli nzito. Katika kauli ya viongozi hao, iliyotolewa jana mjini hapa kwa wanahabari, wamekanusha vikali baadhi ya madai …
Dk. Shein ataka ubakaji utafutiwe ufumbuzi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameutaka uongozi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kulitafutia ufumbuzi wa haraka tatizo la ubakaji ambalo limeonyesha kushika kasi mkoani humo. Dk. Shein aliyasema hayo jana katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo. Katika maelezo …
Zanzibar, jina kubwa!
Na Rungwe Jr. Watanzania tunazidi kufarijika tunapoona majina ya nchi zetu yanatumika maeneo haya ya ughaibuni, kwa watu kufanya biashara na kujikimu maisha yao. Pamoja na hayo ndugu zangu, hii ni changamoto kwetu wote! Kwani Club kama hii si ingekuwa poa sana kama