Breaking News, Chadema wapigwa mabomu Dar

Na Joachim Mushi, Thehabari, Dar es Salaam TAIFA  ambazo mtandao wa dev.kisakuzi.com umezipata muda huu ni kwamba Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Dar es Salaam wamelazimika kuwatawanya vijana wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wanaandamana kuelekea kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, anakoshikiliwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe.  Taarifa zinadai kuwa …

Dk Slaa atangaza mgomo, ni kufuatia kukamatwa wabunge

*Ni kufuatia kamatakamata ya wabunge wa Chadema akiwemo Mbowe *Asema uvumilivu basi, watu waingie mtaani Na Edson Kamukara KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amewataka wafuasi wa chama hicho nchi nzima kuingia mitaani kupinga vitendo vya Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wao wakiwemo wabunge bila kufuata utaratibu. Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku mbili …

Kikombe kingine chaibuka wilayani Mpanda

Na Mwandishi Wetu, Sumbawanga ULE mtindo wa baadhi ya wa kuibuka na kudai wameotesha na Mungu wakiwa usingizini waje kutoa dawa maarufu kama ‘kikombe’ kwa wagonjwa wa magonjwa sugu umeendelea na sasa mganga mwingine kaibuka wilayani Mpanda Mkoa wa Rukwa na kudai ameoteswa na Mungu kufanya kazi hiyo. Bujukano Charles Shashi (44), mkazi wa Kitongoji cha Mkuyuni, Kijiji cha Usevya ameibuka na …

Chadema kwachafuka, Mbowe, Zitto wakamatwa

Na Mwandishi Wetu KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni aliyekuwa akitakiwa kukamatwa kwa amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mjini Arusha amekamatwa jijini Dar es Salaam.  Taarifa zilizoufikia mtandao huu zilieleza Mbowe tayari anashikiliwa na polisi wa jijini Dar es Salaam, kutekeleza amri ya mahakama ya Arusha ambapo Mbowe anakabiliwa na kesi pamoja na viongozi wengine wa …

CCM Arusha maji mazito, hakijaeleweka

Na Janeth Mushi, Thehabari, Arusha MVUTANO baina ya Katibu wa CCM mkoani hapa Mary Chatanda (pichani chini) na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) umeingia sura mpya baada ya uongozi wa chama hicho mkoa kuamua kuitisha kikao maalumu cha Kamati ya Usalama na Maadili. Kikao hicho ambacho kilifanyika jana katika ofisi za CCM mkoani hapa kuanzia majira ya …

Dk Shein amaliza ziara Kusini Pemba

Na Rajab Mkasaba, Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemaliza ziara yake katika mikoa mitano ya Zanzibar na kueleza kuwa Serikali imeamua kuimarisha zao la karafuu ikiwa ni pamoja na kupandisha bei ya zao hilo ili kuwanufaisha wakulima. Dk. Shein ameyasema hayo leo katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji, …