Na Mwandishi Wetu, Unguja RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kusikitishwa kwake na tabia iliyoibuka hivi sasa ya Waislamu kutofautiana na kubughudhiana katika mambo ya uongozi wa misikiti. Dk. Shein aliyasema hayo leo huko Tunduni Wilaya ya Kati Unguja mara baada ya kuufungua msikiti wa Tunduni, hafla ambayo ilihudhuriwa na viongozi …
Zitto, Mnyika wafichua upotoshaji bajeti ya Mkulo
WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, anadaiwa kulipotosha taifa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa kwa lengo la kuwajengea wananchi matumaini hewa yenye kuonyesha serikali inawajali na kusikiliza matatizo yao. Matumaini hayo aliyaonyesha kupitia hotuba yake ya bajeti ya mwaka 2011/2012 juzi ambayo ilionyesha kuwa kutakuwa na nafuu ya maisha wakati hali halisi haipo hivyo. Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa …
CCM yaipa pole Afrika Kusini kwa msiba
Na Mwandishi Wetu CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pole kwa chama cha ANC, kufuatia kifo cha Mama Nontsikelelo Sisulu, mke wa aliyekuwa mpigania uhuru wa nchi ya Afrika Kusini, Walter Sisulu. Akizungumza baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo ya kifo hicho jana Ubalozi wa Afrika Kusini mjini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema, …
Upinzani waiponda bajeti, wasema imejaa upotoshaji
Baadhi ya wabunge waliotoa maoni yao kuhusiana na bajeti hiyo, walieleza kwamba ni bajeti yenye lugha ya kufurahisha na kugusa hisia za watu, ya kinadharia lakini isiyo na ubunifu. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alisema: “Mkulo ametoa maelezo ya kisiasa…serikali imewapiga wafanyakazi changa la macho kwa sababu haijaeleza itapunguza kodi kwenye mishahara kwa asilimia ngapi na wala …
Bajeti 2011/2012, daladala kuumia, pombe, sigara juu tena
Na Said Mwishehe, Dodoma BAJETI ya fedha ya mwaka 2011/2012 imeonesha kutoa matumani makubwa kwa mwananchi wa kawaida kutokana na dhamira ya Serikali kupunguza ukali wa maisha huku ikitangaza vipaumbele vyake ni umeme, maji, miundombinu, viwanja vya ndege, kuinua kilimo cha umwagiliaji na kupanua ajira. Katika bajeti hii mpya Serikali inatarajia kutumia zaidi ya trilioni 13.5 ikiwa ni kiasi kikubwa …
Serikali, sekta binafsi kushiriki ununua mazao
Benjamin Sawe na Beatrice Mlyansi Maelezo-Dodoma SERIKALI itaendelea kushirikisha sekta binafsi ili kushiriki kununua kwa wingi mazao, kuyasindika na kuyasambaza kwa bei nafuu kwenye maeneo yenye upungufu. Akijibu swali Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango lililouliza serikali inampango gani madhubuti kurekebisha kupanda kwa bei za vyakula kuliko uwezo wa wananchi kiuchumi, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu …