KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA DAVID MSUYA NA MUFTI WA TANZANIA

KATIBU Mkuu wa CCM Wilson Mukama akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, Waziri Mkuu huyo mstaafu alipomtembelea Katibu Mkuu, Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makamo Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam, jana (LEO). (Picha na Nkoromo Daily Blog) Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa bin Shaaban Simba akimkaribisha ofisini kwake, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson …

WACHAMBUAJI PAMBA WAGOMA KUNUNUA PAMBA!

Na Baltazar Mashaka, TheHabari, MWANZA. BAADHI ya wachambuaji wa pamba mkoani hapa wametishia kugoma kununua pamba  kupinga kukatwa shilingi 100 kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Pamba nchini (CDTF). Wafanyabiashara hao pia wamepinga wakulima kukatwa kiasi kama hicho cha fedha kuchangia mfuko huo kwa madai kwamba, hauwasaidii kikamilifu wakulima wa pamba kupata madawa ya kuulia …

JESHI LA POLISI ARUSHA KATIKA KASHFA!

Na Janeth Mushi, TheHabari, Arusha JESHI la polisi mkoa wa  Arusha limekumbwa na kashfa nzito mara baada ya kuficha majina ya watu watatu waliouawa baada ya kufanya tukio la utekaji na ujambazi kwa wafanyabiashara watano lililojitokeza juzi majira ya saa 7;00 mchana nje kidogo ya mji wa Arusha.

Rais Kikwete akutana na Mh. Hillary Clinton Ikulu Dar!

Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mheshimiwa Hillary Clinton mara baada ya kufanya mazungumzo ya kiserikali huko Ikulu tarehe 13.6.2011 Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya tete-a-tete na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Mheshimiwa Hillary Clinton huko Ikulu tarehe 13.6.2011. Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Press Conference na Mheshimiwa Hillary Clinton huko Ikulu tarehe 13.6.2011 Rais Jakaya Kikwete …

NCCR-Mageuzi watoa tuhuma zito bungeni

  Na Mwandishi wa Thehabari, Dodoma CHAMA cha NCCR Mageuzi kupitia mbunge wao wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila kimetoa tuhuma nzito za rushwa zinazofanywa na baadhi ya wabunge na mawaziri na kimedai kinawajua viongozi hao kwa majina. Kafulila ametoa tuhuma hizo leo akichangia Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano kuanzia 2011/2016 ambapo alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa …

FFU Dodoma wapambana na wanafunzi UDOM

Na Mwandishi wa Thehabari, Dodoma KIKOSI cha Kutuliza Ghasia (FFU) jana mjini hapa kililazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma Kitivo cha Sayansi ya Jamii na Sanaa ya Lugha ambao waligoma na kufanya maandamano kuelekea Bungeni kwa madai ya kukutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Hata hivyo wanafunzi hao hawakufanikiwa baada ya FFU kutanda karibu …