Thehabari yachaguliwa kushiriki kutafuta blog bora Tanzania
Asante mpenzi na mdau wa Thehabari kwa kuuwezesha mtandao huu kuingia katika mchujo wa kutafuta blog bora Tanzania. Uongozi wa Thehabari unapenda kuwajulisha kuwa mafanikio haya yamepatikana kwa ushirikiano wa kila mpenzi na msomaji wa mtandao huu. Hivyo basi endelea kuuweka kileleni katika shindano hilo kwa kuupigia kura zaidi hapo chini. Kupiga kura tafadhali bofya; www.Tanzanianblogawards.com Ifuatayo ni barua kuchaguliwa …
Mbunge CCM apewa bendera ya Chadema
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Steven Masele (CCM) amelazimika kupokea bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka kwa vijana wa Kata ya Ndala walioamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwa kile kinachodaiwa wamekosa dira ya muelekeo wa kufanya maendeleo. Akipokea bendera hiyo badala ya kadi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Ndala, jana …
Waziri wa Kenya awapasha viongozi Tanzania
Na Anicetus Mwesa WAZIRI wa Nchi Huduma za Jamii wa Kenya, Dalmas Anyango amewataka viongozi wa umma kutojiona miungu watu, na hivyo kuwatumikia wananchi wanaowaongoza. Amesema watumishi wa umma wanapaswa kutambua kuwa wana deni la kuwatumikia wananchi wao, na kwamba kama kuna mtumishi yeyote hayuko tayari kuwahudumia wananchi kwa kazi ambayo aliiomba ni bora sasa akajiengua mwenyewe katika ofisi aliyoko. …
Serikali yawaonya wanaouza ardhi kwa wawekezaji
Veronica Kazimoto na Aron Msigwa, Dodoma 20/6/2011 SERIKALI imewataka wananchi kulinda na kuhifadhi ardhi zao na kuacha tabia ya kuziuza holela kwa wawekezaji bila kufuata kanuni na matakwa ya sheria ya Ardhi. Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Ole Medeye wakati akijibu swali la mbunge wa Mufindi Kusini Mhe. …