Morogoro JESHI la Polisi mkoni hapa limewatahadharisha wakazi wa Manispaa ya Morogoro kutonunua samaki, kwa watu wanaotembeza mitaani kutokana na watu wasiofahamika kumwaga vitu vinavyohisiwa kuwa sumu kwenye Mto Ngerengere. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kamanda wapolisi mkoni hapa Adolphina Chialo alisema watu wasiofahamika walimwaga kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu kwenye mto Ngerengere kwa lengo la kuuwa …
Mkongo wa mawasiliano hauna madhara kiafya-Serikali
Na Lydia Churi-MAELEZO, DODOMA SERIKALI imesema kupitisha mkongo wa taifa wa mawasiliano chini ya nyumba hakuna madhara yoyote kwa afya ya wananchi wanaoishi kwenye nyumba hizo wala kwa nyumba zenyewe. Akijibu swali Bungeni mjini Dodoma leo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga alisema Mkongo wa Taifa hauna madhara yoyote ya kiafya mahali unapopita kwa kuwa hupitishwa chini …
Shibuda aigeuka chadema, aomba posho zibadilishwe jina
Dodoma MBUNGE wa Maswa Magharibi John Shibuda (Chadema) amewaugeuka wabunge wa chama hicho kwa kuitaka Serikali kuongeza posho za wabunge badala ya kuziondoa. Amesema kuwa kwa majukumu ambayo yanafanywa na wabunge hasa wa aina yake ambaye ni mbunge kwa ajili ya maslahi ya jamii na si binafsi ni vema posho zikaendelea kutolewa na kutaka ziitwe malipo ya mwia. Shibuda alitoa …
MADAKTARI, WAUGUZI WATAKIWA KUOKOA MAISHA YA WAGONJWA
Na Aron Msigwa – MAELEZO 28/6/2011, Moroni, COMORO Madaktari na wauguzi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaowahudumia. Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya El Maarouf iliyoko mjini Moroni nchini Comoro kuona namna huduma …
Benki ya dunia kuendelea kuisaidia Zanzibar
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar BENKI ya Dunia imeahidi kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miradi yake ya maendeleo na kueleza matumaini yake kutokana na juhudi zinazochukuliwa na serikali katika kuimarisha uchumi na huduma za kijamii. Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, John Mclntire aliyasema hayo leo wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kuaga na kuzungumza na Rais …