Bunduki haiwezi kumaliza matatizo yetu – JK

Malabo, Equatorial Guinea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameziambia Sudan na Sudan Kusini kuwa bunduki haiwezi kutoa majawabu ya mvutano kati ya pande hizo ambazo zitatengana na kuwa nchi mbili tofauti Julai 9, mwaka huu, 2011, wakati Sudan Kusini itakapokuwa Taifa Huru. Mheshimiwa Kikwete amesema kuwa njia pekee ya kupata majawabu sahihi ya mvutano …

Kikwete:Ukosefu wa ajira kwa vijana wa Afrika ni bomu linalosubiri kulipuka!

Malabo, Equatorial Guinea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ukosefu mkubwa wa ajira na nafasi za kujiendeleza kwa vijana wa Afrika ni bomu linalosubiri kulipuka na linalohitaji majawabu ya haraka kulizuia lisilipuke. Rais Kikwete pia amesema kuwa ni wajibu na jukumu la viongozi wa Afrika kuwekeza ipasavyo katika vijana ili kuwawezesha kutimiza nafasi …

Rais Kikwete aombwa kuendelea kuongoza ALMA

Malabo, Equatorial Guinea Viongozi  wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wamemwomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuendelea kuongoza umoja wa wakuu hao unaopambana na ugonjwa wa malaria – African Leaders Malaria Alliance (ALMA) wakati wanajiandaa na kuangalia jinsi ya kumpata kiongozi mwingine wa umoja huo. Rais Kikwete amekubali ombi hilo, lakini kwa masharti kuwa anaendelea kuwa Mwenyekiti wa ALMA …

Mh. Kikwete in Malabo for AU Summit

Malabo, Equatorial Guinea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Juni 30, 2011, alikuwa miongoni mwa viongozi wa Serikali na nchi 53 za Afrika walioshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ulioanza katika mji mkuu wa Equatorial Guinea wa Malabo.

India mbioni kudhibiti idadi ya watu

MPANGO huo mpya wa uzazi unanuia kuwashawishi wanawake na wanaume kukubali njia ya kumaliza kabisa nguvu za mayai ya uzazi. Wanaokubali watapokea zawadi ya gari lipya miongoni mwa zawadi nyingine. Tata nano, ndio gari lenya bei rahisi sana duniani lakini kulingana na kampeni hiyo, bila shaka kuna uwezekano likawa maarufu zaidi nchini India katika siku chache zijazo. Dakatri Sitaram Sharma …