WAZIRI MKUU ATAKA UHARAMIA UPEWE MSUKUMO NA AU

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema suala la uharamia linahitaji kupata nguvu zaidi ya kukabiliana nalo kutoka ngazi ya Umoja wa Afrika (AU) na lisichukuliwe kuwa ni jambo linaloweza kutatuliwa na Serikali ya Tanzania peke yake. Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Julai 05, 2011) nyumbani kwake, Oysterbay, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Mjumbe Maalumu wa …

Upinzani waitaka BAE ilipe haraka chenji ya Tanzania

Dodoma KAMBI ya Upinzani Bungeni, imeunga mkono juhudi za Serikali za kupinga nia ya, Kampuni ya BAE systems ya Uingereza ya kutaka kulipa fedha za Rada sh. bilioni 75.2 za Tanzania kupitia kwa Asasi zisizo za kiserikali za Uingereza. Pia imeitaka kampuni hiyo ya BAE systems kulipa fedha hizo haraka iwezekanavyo, na kutaka wahusika wote wa kashfa ya rada, akiwemo …

Tanzania itanufaika na GS1 kibiashara-Dk Bilal

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi huduma mpya ya Mfumo wa Utambuzi wa Bidhaa Tanzania, (Global Standard 1 ), wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Julai 04, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR Na Joachim Mushi MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dk. Gharib Bilal amesema …

WAZIRI MKUU KWENDA KOREA KUSINI LEO

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda anatarajiwa kuondoka nchini kesho (Jumanne, Julai 05, 2011) kwenda Korea Kusini ambako atazindua meli ya uchimbaji mafuta iitwayo Poisedon ambayo inajengwa katika bandari ya Geoje. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, uzinduzi huo utafanyika Ijumaa, Julai 8, 2011 katika mji wa Busan ambao uko kusini mwa nchi …

Mbunge aufagilia utendaji wa Serikali

Mbunge Neema Mgaya Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Viti Maalumu CCM, Neema Mgaya, ameipongeza serikali kwa kuwawezesha vijana wanaosoma elimu ya juu kupata mikopo na kuendelea na masomo yao. Akichangia hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, mwishoni mwa juma, Neema, alisema serikali imetumia sh. bilioni 185 kwa ajili ya kuwakopesha vijana 96,328, hapa nchini. Sambamba na hilo, mbunge huyo anayewawakilisha …

Rais Ondimba wa Gabon aomba msaada wa kufundishwa Kiswahili!

   Na Salva Rweyemamu Tanzania imeombwa kuisaidia Gabon kubuni, kuanzisha na kusimamia mitaala inayofaa kuanzisha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika shule za nchi hiyo kufuatia uamuzi wa Serikali ya Gabon kuanza kufundisha lugha hiyo tokea elimu ya msingi. Aidha, Rais wa Gabon, Mheshimiwa Ali Bongo Ondimba amemwomba binafsi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho kusaidia …