NGELEJA: AJIRA KUONGEZEKA LINDI NA MTWARA

WAZIRI wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja amesema uwekezaji unaoendelea hivi sasa katika mikoa ya kusini ni kiashiria kizuri juu ya kukua kwa uchumi wa mikoa hiyo na hasa katika bandari ya Mtwara. Alikuwa akitoa ufafanuzi leo mchana (Alhamisi, Julai 07, 2011) kuhusu uamuzi wa kampuni ya Petrobas ya Brazili kuweka meli yake katika bandari ya Mtwara wakati ikifanya …

PINDA: SERIKALI HAITAINGIA GHARAMA WAKATI WA UTAFITI WA MAFUTA NA GESI

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali ya Tanzania haitaingia gharama zozote wakati meli ya Poisedon itakapokuwa inafanya uchunguzi wa mafuta na gesi katika pwani ya Tanzania. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Julai 07, 2011) mara baada ya kutembelea eneo la viwanda vya kujenga meli (ship building area) ili kuona hatua mbalimbali za ujenzi wa meli na kuikagua meli ya …

Wajumbe wa Bodi ya NSSF watembelea banda la NSSF

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF, Abubakari Rajab (wa tatu kushoto) pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo wakiangalia mfano wa daraja la Kigamboni linalotarajiwa kujengwa na shirika hilo (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau akitoa maelezo kwa wajumbe hao walipotembelea banda la NSSF kwenye maonesho 35 ya Biashara Kimataifa Saba Saba Dar es Salaam …

Mbunge Chadema aitaka Serikali kutaja mshahara kima cha chini

Na Mwandishi wa Thehabari Dodoma Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA, Rose Kamili MBUNGE wa Viti Maalumu CHADEMA, Rose Kamili ameitaka Serikali kueleza kinagaubaga kima cha chini cha mishahara kimepanda kwa kiasi gani na si kutoa maelezo ya jumla. Kamili alitoa hiyo Bungeni jana wakati akichangia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ya Makadirio …

Rais Kikwete kutembelea Saba Saba leo

Na Joachim Mushi RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete leo anatarajia kutembelea Maonesho ya 35 ya Biashara Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kwamujibu wa taarifa iliyopatikana jana kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Rais Kikwete atakuwa ni miongoni mwa wageni mashuhuli ambao watatembelea maonesho hayo leo kushuhudia …