PINDA AWAALIKA WAWEKEZAJI WA GESI ASILIA KUTOKA NJE

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema umefika wakati kwa wawekezaji wa kimataifa kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika miundombinu ya kusafirisha gesi asilia kama njia mojawapo ya kusaidia kukuza uchumi wa Tanzania. Amesema kupatikana kwa gesi nyingi katika ukanda wa pwani ya kusini mwa Tanzania kunatoa fursa ya wawekezaji kuanza kufikiria ujenzi wa mabomba ya gesi ili bidhaa hiyo iweze kutumika viwandani, …

Tigo wamzawadia pikipiki ya mizigo mshindi mwingine

Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (kushoto) akizungumza na mshindi wa pili wa droo ya pikipiki ya magurudumu matatu kwa njia ya simu alipokuwa akichezesha droo hiyo, kulia ni Mratibu wa Matukio kutoka Tanzania Solid Limited, Catherine Kasimbagi. Na Joachim Mushi KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Tigo imetoa zawadi ya pili kwa mshindi wa pikipiki ya miguu mitatu aina …

Ziara ya Waziri Kabaka ndani ya mabanda ya Wizara ya Fedha

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye Banda la Wizara ya fedha kutembelea idara mbalimbali zilizo chini ya Wizara hiyo. Waziri akianza safari ya kutembelea mabanda ya Wizara ya fedha, kushoto anaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elizabeth Nyambibo. Waziri Kabaka akitembelea banda la Mfuko wa Pensheni kwa …

Bodi ya Maziwa kudhibiti maziwa ya nje

Meneja wa Huduma ya Masoko wa Bodi ya Maziwa nchini, Mayasa Simba Na Joachim Mushi BODI ya Maziwa Tanzania imesema imeanza kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) kuhakikisha inaratibu kiwango cha uingiaji wa maziwa nchini ili kulinda maziwa ya ndani. Kauli hiyo ilitolewa jana katika Maonesho ya 35 ya Biashara Kimataifa …

CCM inatekwa na matajiri – Sumaye

Fredrick Sumaye Moshi WAZIRI Mkuu mstaafu wa Awamu ya Tatu, Fedrick Sumaye amesema zipo ishara ambazo zinajitokeza ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambazo kama hazitaangaliwa vizuri zitakivuruga chama hicho na nchi kwa jumla. Sumaye aliyasema hayo jana akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Pasua, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo alisema moja ya ishara hizo ni kuwepo …

Rais Kikwete kujenga masoko mahususi ya bidhaa

Rais Jakaya Kikwete Na Joachim mushi SERIKALI imesema itahakikisha kabla ya kuondoka madarakani inajenga maeneo maalumu na masoko mahususi ya bidhaa mbalimbali ili kuwarahisishia wajasiria mali kupata soko la bidhaa hizo muda wote, tofauti na kutegemea maonesho ya Saba Saba pekee. Kauli hiyo ilitolewa jana na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizungumza na wanahabari ndani ya Maonesho ya 35 ya Biashara …