*Asema hataki chai, anataka umeme Dodoma ILE siku iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wabunge imewadia ambapo mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango (CCM), amekuwa wa kwanza, kumtupia makombora Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja mara baada ya waziri huyo kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2011/2012 ya wizara yake. Kilango akitoa mchango wake amegoma kuunga …
Makamba na Shekifu, uso kwa uso Bungeni!
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Januari Makamba akizungumza jambo na kusalimiana na Mbunge wa Jimbo la Lushoto Henry Shekifu mara baada ya kuwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2010/2011 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/2012. PICHA NA MAGRETH …
Dk Chami azungumza na wafanyabiashara wa Japan
Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Cyril Chami akiwa katika mazungumzo na kiongozi wa kundi la wafanyabiashara kutoka Japan waliomtembelea ofisini kwake jijini dsm leo. Wafanyabiashara hao wameonesha nia ya kuwekeza katika maeneo mbali mbali nchini. Kutoka kushoto waliosimama. Balozi wa Japan hapa nchini Bw Hiroshi Nakagawa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Cyril Chami wakiwa katika picha ya …
CCM kujadili tathmini ya kujivua gamba Mbeya kesho
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mbeya kinatarajia kufanya maandamano makubwa, kesho Jumapili Julai 16, yatayofuatiwa na mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya Luanda Nzovwe, jijini Mbeya. Maandamano hayo yatakayoanzia eneo la Mafiati na kuishia viwanja vya Luanda Nzovwe, yatawashirikisha wana-CCM, wapenzi na wananchi wa jiji …
Matukio Mkutano wa Wahariri Arusha uliodhaminiwa na SBL
Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Boniface Meena (katikati) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda baada ya awamu ya kwanza ya mkutano wa wahariri wa habari nchini unaoendelea mjini Arusha. Baadhi ya wadau wanaohudhuria mkutano wa wahariri mjini Arusha wakiwa katika mapumziko na kutafakari mada zilizotolewa katika awamu ya asubuhi …
Mbunge Chadema ataka muungano uvunjwe
Dodoma MBUNGE wa Viti Maalumu, Mwanamrisho Abama (CHADEMA), ameiomba Serikali kuridhia Muungano uvunjwe. Abama alitoa kauli hiyo jana wakati akiuliza swali la kwa Waziri Mkuu, Abama alimnukuu Hayati, Abeid Karume ambaye aliufananisha muungano na koti. “Kabla sijauliza swali langu nomba nimnukuu, Hayati Abeid Karume, alisema Muungano wetu ni kama koti, likikubana waweza kulivua mimi naona ni wakati muafaka wa kulivua …