JK: nchi za Africa zinahitaji misaada ya maendeleo

Rais Jakaya Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni kweli nchi za Afrika bado zinahitaji misaada ya maendeleo lakini wajibu wa kuendeleza nchi hizo unabakia mikononi mwa nchi hizo na siyo kwa mtu mwingine yoyote wakiwamo wafadhili. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa wakati umefika kwa Tanzania na Afrika Kusini kutumia uhusiano wa …

Rais Kikwete amtumia rambirambi Mkuu wa Majeshi

Jenerali Davis Mwamunyange. Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange kufuatia kifo cha Brigedia Jenerali Ally Abdallah Sinda kilichotokea ghafla jijini Dar-es-Salaam tarehe 17 Julai, 2011 asubuhi katika Hospitali ya Jeshi, Lugalo (521 KJ). “Tumempoteza mpiganaji hodari katika ulinzi wa nchi yetu na pia katika kupigania afya za Watanzania mbalimbali waliofika katika …

Siku timu ya soka ya Bunge ilivyonyakua Kombe!

Mbunge wa Sengerema, Mh. William Ngeleja akiwa anachekelea huku amenyanyua Kombe la ushindi juu, washrika wengine wakiwa wanashangilia. Jezi nambari Tano mgongoni Mh. Ngeleja akiyoyoma na kikombe huku wadau wakimshangilia. Mh. Ngeleja akiondoka na Kikombe huku wadau wakifuata. Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Adam Malima akiungana na Mh. Malima kusheherekea ushindi wao dhidi ya timu …

Wafahamu baadhi ya wachezaji hatari wa kikosi cha PSPF!

Wachezaji hatari wa timu ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Rahim Hashim na Sudi Hamza wakiwa mazoezini  Wachezaji wa mpira wa Pete Safina, Valley, Mariam Lisasi, Mariam Muyovela, Mwajaa, Munisi na Salome Makala. Picha na mdau Rahim Hashim wa Dodoma.

Yaliyojiri katika mechi kati ya Bunge na PSPF huko Dodoma!

Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wakipata maelekezo ya mwisho kutoka kwa kocha wao katika mazoezi yaliofanyika jumamosi asubuhi katika kiwanja cha Jamhuri Mjini Dodoma kabla ya mpambano wao na Timu ya Bunge. Kocha akiendelea kutoa dozi Wachezaji wakiendelea kumsikiliza kocha wao kwa umakini mkubwa.       Picha kwa …

Ngeleja, Katibu wake ‘matatani’, wabunge wagomea bajeti yake

Waziri Ngeleja akizungumza bungeni. Dodoma, IDADI kubwa ya wabunge wakiwemo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameikataa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, na Serikali kuomba ikajipange upya kabla ya kuiwasilisha tena bajeti hiyo bungeni. Mbali na Waziri Mkuu Pinda kuiondoa bajeti hiyo jana bungeni Dodoma, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, David …