Waziri Mkuu awataka wabunge kuchangamkia maabara

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema wakati Serikali inajipanga kutekeleza mpango wa kuimarisha masomo ya sayansi shuleni, meza ya maabara inayohamishika inaweza kutumika kupunguza tatizo la uhaba wa maabara katika shule za sekondari nchini. Alitoa kauli hiyo jana (Julai 20, 2011) mara baada kuzindua rasmi meza ya maabara inayohamishika (mobile science laboratory table with equipment) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma. …

Basi la Hood lapata ajali Mikumi, 10 wahofiwa kufa

WATU 10 wanahofiwa kupoteza maisha huku 34 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Hood namba T.762 AVL aina ya Scania kuteketea kwa moto. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Joseph Lugila alisema ajali hiyo ilitokea katika Mbuga ya Mikumi baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso la lori lilobeba mafuta ya kupikia lililokuwa likitoka Morogoro kuelekea Iringa …

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katika Ziara Rasmi ya kitaifa Afrika ya Kusini

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Ulinzi la Afrika ya Kusini wakati wa mwanzo wa Ziara yake Rasmi ya kitaifa nchini Afrika ya Kusini .Mawaziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na Tanzania Bernard Membe na Bi. Maite Nkoana Mashabane wakibalishana mikataba ya kuanzishwa kwa Tume ya Ushirikiano(Bi-National …

Chadema yasema vyama vyote vinafanya siasa vyuoni

Dodoma, MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), amesema siasa vyuoni hazitakoma, endapo Serikali itashindwa kuwatimizia wanafunzi haki zao. Alisema kila chama kinafanya siasa vyuoni na siyo kukitupia lawama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo pekee, kwamba kinafanya siasa vyuoni. Mbilinyi alitoa kauli hiyo bungeni jana, wakati akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ya …

Wabunge wa CCM walivyovutana kabla ya kuiondoa bajeti ya Ngeleja bungeni, wapendekeza bosi Tanesco aadhibiwe

Baadhi ya wabunge wa CCM wakiwa bungeni Dodoma. Dodoma VUGUVUGU la kuondolewa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, lilianzia ndani ya kikao cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo walivutana vikali kabla ya kuazimia kuitoa bungeni bajeti hiyo. Vyanzo vya habari kutoka katika mkutano huo uliofanyika mjini Dodoma siku moja kabla ya Serikali kuiondoa bungeni bajeti hiyo; …

Naibu Spika wa Bunge amzika bibi yake

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akiwa na mkewe Dk. Fatuma akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu, Luhama Chonya ambaye ni bibi mzaa mama, aliyemlea Naibu Spika. Mazishi hayo yalifanyika jana kijijini Ibwaga, wilayani Kongwa, Dodoma. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akitoa heshima za mwisho kwa …