David Jairo Dodoma KATIBU Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo amemsimamisha kazi Katibu wa Nishati na Madini, David Jairo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili za kuchangiza zaidi ya sh. bilioni moja kinyemela. Jairo anaanza kutumikia adhabu hiyo leo, huku akimpisha Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi wa fedha zinazodaiwa kuchangishwa na Katibu Mkuu huyo ili kuwashawishi wabunge waipitishe …
Simba yanga kupambana tena Agosti 13
MAHASIMU wa jadi timu za mpira wa miguu za Simba na Yanga zote za Dar es Salaam, zinatarajia kukutana tena Agosti 13, 2011 mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mchezo huo utakuwa ni wa ufunguzi wa kuzindua msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom, inayotarajia kuanza rasmi Agosti 20, 2011. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa mtandao wa …
Wizara ya Nishati na Madini inaliaibisha Taifa-Wanaharakati
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP MUUNGANO wa Asasi za Kiraia zinazotetea Usawa wa jinsia, haki za binadamu, maendeleo na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct), umepokea kwa mshtuko, mshangao na masikitika tuhuma za Katibu Mkuu, Wizara ya Madini na Nishati, za kuandaa mpango wa kukusanya pesa idara na wakala walio chini ya wizara yake, kwa ajili ya ‘kuhonga’ wabunge ili wapitishe bajeti …
Serikali yangu haitaweka lami Serengeti- Kikwete
Rais Jakaya Kikwete Pretoria, Afrika Kusini RAIS wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema Serikali yake haikusudii kujenga barabara ya lami kukatisha mbuga maarufu duniani ya Serengeti iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Tanzania. Rais Kikwete amesema kuwa kama yupo kiongozi ambaye amethibitisha wakati wote wa uongozi wake kuwa mtetezi mkubwa wa mazingira na kulinda mbuga za wanyama basi ni yeye mwenyewe. “Serengeti …
Rais Kikwete ashawishi wawekezaji wa zabibu kuja Tanzania
Zao la zabibu Pretoria, Afrika Kusini RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete Julai 20, 2011, alitumia siku ya pili ya ziara yake ya kihistoria Afrika Kusini kwa kutembelea na kushawishi wawekezaji wa kilimo cha zabibu na utengenezaji divai kutoka nchi hiyo kuwekeza katika kilimo cha zao hilo mkoani Dodoma. Aidha, Rais Kikwete ametembelea Kisiwa cha Robben, kilichoko …
Pinda asema taarifa za Jairo kujiuzulu ni uzushi
David Jairo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dodoma, TAARIFA zilizotolewa jana na gazeti moja la kila siku kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo amejiuzuru si za kweli Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amethibitisha hilo. Waziri Pinda amesema, kama ilivyo kwa Watanzania wengine, naye amesikia taarifa za, Jairo kujiuzulu kwenye vyombo vya habari na si …