Katibu wa NEC CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza baada ya kuzindua tawi la wanachama wa CCM la wasomi wa Chuo Kikuu cha Tumaini (SIMCO), katika mkutano uliofanyika katika mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro, jana. Wengine kutoka kushoto, wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo Swaijaro na kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro …
Loveness ndie Vodacom Miss Kanda ya Mashariki 2011
Vodacom Miss Eastern Zone 2011, Loveness Flavian (katikati) akipunga mkono akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili, Asha Saleh (kushoto) na Mariaclara Mathayo aliyeshika nafasi ya tatu, baada ya warembo hawa kutangazwa washindi wa shindano hilo. Loveness aliwashinda warembo wengine 10.Warembo wakipita jukwaani na vazi la ufukweni katika shindano la Vodacom Miss Kanda ya Mashariki, iliyofanyika mjini Morogoro …
Ikulu yamteua mrithi wa Jairo Nishati na Madini
KATIBU Mkuu Kiongozi, Phillemon L. Luhanjo amemteua Eliakim Chacha Maswi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Luhanjo amefanya mabadiliko hayo jana baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, David Jairo, kupewa likizo kwa muda, ili kupisha uchunguzi katika ofisi yake, ambapo inadaiwa wizara hiyo ilizichangisha fedha taasisi zake kwa lengo la kutumika kushawishi bajeti ya wizara ipitishwe …
WAZIRI WA AFYA NA HUDUMA YA WATU WA MAREKANI
Rais Jakaya Kikwete (Kushoto) akichukua nafasi muda mfupi kbla ya mazungumzo na wajumbe wa Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF), kwenye ukumbi wa karimjee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ikulu) Rais Jakaya Kikwete (Kulia) na Balozi wa marekani nchini, Alfonso E. Lenhadrt (Kuloa) wakishuhudia wakati mke wa rais, Mama Salma, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa waziri wa Afya na …
JK akutana na waziri wa afya wa Marekani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya na Huduma ya Watu wa Marekani Mheshimiwa Kathleen Sebelius. Rais Kikwete ameishukuru Serikali ya Marekani kwa msaada wake mkubwa unaotoa kwa Tanzania katika sekta ya Afya. “Marekani inaongoza kwa msaada wake katika sekta ya Afya, tunashukuru sana na kuja kwako Tanzania kumetupa nafasi ingine ya kusema tunashukuru”. …
Mwanahabari mkongwe Mkina apata ajali
Na Mwandishi Wetu Mwanahabari mkongwe nchini, Simon Mkina ambaye amewahi kuwa mhariri wa magazeti mbalimbali ndani na nje ya Tanzania amepata ajali ya gari. Mkina amepata ajali hiyo jana usiku jijini Dar es Salaam akitokea katikati ya mji kuelekea nyumbani kwake Bunju, baada ya gari lake namba T 588 BPN aina ya Daihatsu kugonga nguzo ya umeme alipokuwa akijaribu kukwepa …