Arusha kwachafuka tena, FFU wapiga mabomu, virungu

Baadhi ya waandamanaji wakiimba na kucheza kabla ya kuzuka kwa vurugu na FFU kulazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi. Mwandishi Wetu, Arusha MADEREVA wa daladala (maarufu kama vifodi) mkoani Arusha jana walifanya mgomo wakupinga kitendo cha kutozwa fedha kiasi cha Sh 5,000 hadi 10,000 na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani hata kama magari yao hayana makosa. Walidai endapo baadhi …

Mamia wamuaga Danny Mwakiteleko Dar es Salaam

‘Pokea saluti mpiganaji, Danny Mwakiteleko’ baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mwakiteleko. Na Mwandishi Wetu MWILI wa Marehemu, Danny Mwakiteleko umeagwa leo nyumbani kwake Tabata Chang’ombe jijini Dar es Salaam na mamia ya waombolezaji wakiwemo viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi. Baada ya taratibu za kutoa salamu za mwisho …

UVCCM wawalaani wanaojilimbikizia madaraka CCM

Benno Malisa Na Mwandishi Wetu, Dodoma BARAZA Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), limelaani kitendo cha wajumbe wa Halmashauri Kuu NEC ya CCM kujilimbikizia madaraka. UVCCM imependekeza wajumbe wa NEC, wasiwe na madaraka zaidi ya moja kwenye maamuzi ngazi ya kitaifa. Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa alitoa tamko hilo mjini hapa jana, katika …

Wanawake wawili wachinjwa Magu

IGP, Said Mwema Na Mwandishi Wetu, Magu WANAWAKE wawili wameuawa kikataili kwa kuchunjwa katika matukio mawili tofauti wilaya ya Magu, mkoani Mwanza, Kwa kile kinachodaiwa ni imani za kishirikina. Jeshi la Polisi wilayani Magu, limethibitisha katika taarifa zake kutokea kwa matukio yote mawili, na kueleza yametokea katika vijiji vya Mwakiloba na Lutubiga, Kata ya Lutubiga wilayani humo, usiku wa kuamkia …

Kikwete awakumbuka Prof Mushi na Mwakiteleko

Marehemu Danny Mwakiteleko RAIS Jakaya Kikwete amemtumia salaam za rambirambi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala kufuatia kifo cha Mhadhiri Mwandamizi Prof. Samuel S. Mushi wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala. Katika taarifa hiyo pia Kikwete amempa pole Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Limited, Hussein Mohamed Bashe kufuatia kifo cha …

Mukama aiponda CCM, adai viongozi ni ‘waroho’ wa madaraka

Katibu Mkuu wa CCM, Willson Mukama Dodoma, KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Willison Mukama amekiponda chama chake kwa kusema viongozi wengi ndani ya chama hicho ni ‘waroho’ (tamaa) wa madaraka. Mukama alitoa kauli mjini Dodoma jana kwenye Ukumbi wa Halmashauri Kuu CCM, wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM). Hivyo akasema …