Breaking News: Mbunge wa Chadema atolewa bungeni

Mbunge Wenje Dodoma, HABARI zilizotufikia muda huu kutoka bungeni mjini Dodoma ni kwamba; Mbunge wa Ilemela kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ezekiel Wenje ametolewa nje ya Bunge katika kikao kinachoendelea hivi sasa mjini Dodoma. Wenje ametolewa nje ya bunge na Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba ambaye ndiye anayeongoza kikao hicho, baada ya kuvuana huku akihoji kuwa …

Jalada la Chenge utata mtupu

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge HATIMA ya jalada la uchunguzi dhidi ya Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, bado ni kizungumkuti, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Elieza Feleshi, kusisitiza jana kuwa mpaka sasa halijafika ofisini kwake. Lakini alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, alisema: “Kama hajalipata, atalipata …

Umeme waligawa baraza la mawaziri

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda *WANYOSHEANA VIDOLE KUMTAFUTA MCHAWI KAULI tofauti zinazotolewa na viongozi wa Serikali, akiwamo Rais Jakaya Kikwete na baadhi ya mawaziri kuhusu suala la mgawo wa umeme, zinaonyesha kutokuwapo uwajibikaji wa pamoja katika Baraza la Mawaziri.Uchambuzi uliofanywa na gazeti hili kuhusu sakata la tatizo sugu la mgawo wa umeme nchini unebaini kwamba, kauli za viongozi hao wa Serikali …

Maadui wa Serikali si Chadema, niwatendaji-Lusinde

Livingstone Lusinde Dodoma MBUNGE wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), amewalipua watendaji wa umma kwa kueleza kuwa ndiyo maadui wakubwa wa Serikali na siyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Amesema mipango yao isiyotekelezeka ndiyo inasababisha wananchi wakose imani na Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lusinde alitoa kauli hiyo bungeni, wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Makadirio ya Mapato …

Veta shirikianeni na wawekezaji-Kikwete

Rais Jakaya Kikwete Na Mwandishi Maalum, Mtwara RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameutaka uongozi wa Chuo cha Ufundi Stadi Kanda ya Kusini (VETA) kuwa tayari kupokea walimu na vifaa ya kisasa vinavyoletwa na wawekezaji kwa ajili ya sekta ya gesi na mafuta. Rais ametoa kauli hiyo jana mkoani Mtwara alipotembelea chuo hicho kwa ajili ya kuwaeleza nafasi iliyopo na makubaliano yaliyofikiwa …

Matukio Ya Bungeni Dodoma Leo

Naibu waziri Ofisi  ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri  akijibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi Dkt. Anthony Mbassa (hayupo pichani) kuhusu Serikali kugawa maeneo mapya katika wilaya hiyo wakati wa kipindi cha Maswali na majibu Bungeni leo mjini Dodoma. Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda kulia akimsikiliza waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. …