Serikali yamwaga bil 31 Masasi, ni kwenye mradi wa maji

SERIKALI imetenga sh. bilioni 31 kwa ajili ya mradi wa Mbwinji wilayani Masasi utakaohudumia pia wilaya ya Nachingwea. Rais Jakaya Kikwete alisema hayo jana mjini Masasi katika uwanja wa sabasaba alipokuwa akihutubia wananchi. Mradi huo mkubwa ambao chanzo chake cha maji ni Mto Nanguu unagharamiwa na serikali unatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka 2012. Rais yuko mkoani Mtwara kuwashukuru wananchi kwa …

Wabunge wa Chadema watolewa bungeni

Askari wa Bunge wakiwasindikiza wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu (kulia) , Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) na Godbless Lema (wa pili kushoto) kuondoka nje ya viwanja vya Bunge mara baada ya Naibu Spika, Job Ndugai (hayupo pichani) kuwaamuru watoke ndani ya Bunge kwa kile kudai wamevunja kanuni za Bunge. Wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akiwasindikiza. …

Fedha za pembejeo zawatokea ‘puani’ maofisa Chato

Chato, MAOFISA wanne kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Kagera wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutafuna fedha za pembejeo za kilimo zilizotakiwa kupewa wakulima. Kati ya waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo yumo Mwanasheria wa Halmashauri hiyo, Robert Matungwa pamoja na wakala wa usambazaji pembejeo. Watuhumiwa wote walisomewa mashtaka hayo jana mjini hapa na mwendesha mashtaka wa polisi wilayani hapa, …

Breaking News: Ajali mbaya Moshi, 11 wafa 22 wajeruhiwa

Moshi, Taarifa zilizotufikia muda huu ni kwamba; ajali mbaya imetokea mjini Moshi katika barabara ya Kibosho ambapo magari takribani manne yamehusika katika ajali hiyo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio jumla ya watu 11 hadi sasa wamepoteza maisha na wengine 22 kujeruhiwa. Chanzo chetu cha habari kinasema ajali hiyo inadaiwa kusababishwa na basi dogo aina ya Fuso, ambalo …

Kamati ya Wanafunzi Ustawi wa Jamii yazungumza na wanahabari Dodoma

JULAI 21, 2011, Taasisi ya Ustawi wa Jamii ilifunga masomo (kufunga Chuo) kutokana na mgogoro baina ya Menejimenti na Wahadhiri. Mgogoro huo ambao Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo, Mlwande Madihi alisema umesababisha mgomo usio halali wa wahadhiri, umekuwa na madhara makubwa kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kukosa malazi na kushindwa kujikimu kimaisha huku wengine muda wao wa ruhusa kazini …

SARA DUMBA ASIFU JUKWAA LA ALIZETI

SARA DUMBA Na William Macha-Iringa MKUU wa Wilaya ya Njombe, Sara Dumba amelimwagia sifa Jukwaa la Alizeti lililozinduliwa mkoani Iringa, kupitia mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) lilowakutanisha wadau anuai wa masuala ya kilimo na tafiti. Akizungumzia jukwaa hilo, Dumba amesema wakulima wa alizeti mkoani Iringa kwa kipindi kirefu wamekuwa wakizalisha mazao kwa uzoefu, lakini sasa wanapaswa kutumia nyenzo za …