Wafanyabiashara wa vitunguu saumu eneo la Kariakoo Na Mwandishi Wetu WAFANYABIASHARA wasambazaji wa vitunguu saumu jijini Dar es Salaam wameulalamikia utaratibu mpya wa tozo za ushuru kwa bidhaa hiyo, unaofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, ambao umepandisha kodi kwa kiasi kikubwa tofauti ilivyokuwa awali. Malalamiko hayo yametolewa jana jijini Dar es Salaam kwenye soko la wafanyabiashara hao eneo la …
CCM sasa ‘yaingilia’ utendaji wa EWURA
Na Joachim Mushi CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezipinga sababu zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA), za kupandisha kodi ya mafuta ya taa kwa kisingizio cha kudhibiti vitendo vya uchakachuaji vilivyokuwa vimeshamiri. Madala CCM imeiagiza Serikali kuhakikisha inatafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa nchini, kwa kuwa ndiyo nishati inayotumiwa na wananchi …
CCM yaridhia kuondoka madarakani kwa Rostam, yataka wengine wafuate nyayo
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Willson Mkama,akisoma utaratibu wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika hivi karibuni Dodoma,(wa pili kulia) Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete, makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Amaan Abeid Karume, Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamatiu Kuu ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein, wakisikiliza kwa …
‘Maiti’ aamka mochwari Afrika Kusini
Afrika Kusini, RAIA mmoja wa Afrika Kusini ameamka na kujikuta yupo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti mwishoni hivi karibuni, na kuanza kupiga kelele akitaka wahudumu wa chumba hicho wamtoe huku wao wakihofu na kudhani ni mzimu. Familia ya mtu huyo iliamua kutoa taarifa mochwari baada ya kudhani amekufa kwa kile kushindwa kumwamsha Jumamosi usiku na hivyo kuwasiliana na ofisi moja …
Mnyika aelezea ufisadi uliofanyika mradi wa UDA
TAREHE 27 Julai 2011 vyombo mbalimbali vya habari vimemnukuu Meya Wa Jiji la Dar es salaam Dk. Didas Masaburi akieleza kilichoitwa maamuzi ya Baraza la Madiwani wa Jiji kuhusu kuvunja uongozi wa Shirika la Usafiri Dar es salaam (UDA) na kuunda kamati ya kuchunguza matatizo katika shirika hilo. Tarehe 28 Julai 2011 vyombo mbalimbali vya habari vimemnukuu Meneja wa UDA, …
RAIS KIKWETE KUFUNGUA MAONESHO YA NANE NANE
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kesho, (Agosti Mosi, 2011) anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Wiki ya Sherehe za Nane Nane na Maonesho ya Kilimo mwaka huu kwenye Uwanja wa Maonesho ya Kilimo wa Nzuguni, Dodoma. Shughuli kuu za Rais katika ufunguzi huo itakuwa ni kufungua Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane kwa hotuba rasmi …