Na Paul Sarwatt, Arusha Waliokunywa wapimwa baada ya siku 90 Matokeo yaonyesha bado wana virusi Wailaumu Serikali ‘kubariki’ kikombe cha Babu MACHI 20 mwaka huu, Mwenyekiti wa Mtandao wa Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (TANOPHA+), Julius Kaaya alikuwa safarini na wenzake 14 wanaoishi na virusi hivyo kwenda kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro, kupata tiba ya “kikombe” cha Mchungaji Ambilikile …
Zao la alizeti linaweza kukuza uchumi wa Tanga
Na Ngusekela David, Tanga MKUU wa Wilaya ya Handeni, Seif Mpembenwe amesema wakulima wa alizeti wataweza kuinua kipato chao mara dufu endapo watalima zao hilo la alizeti kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora. Mpembenwa alisema hayo mjini hapa alipokuwa akifungua kikao cha pili cha jukwaa la wadau wa alizeti wilayani Handeni, ambalo limeundwa kwa lengo la kuwaunganisha wadau wa zao …
Maonyesho ya Nane Nane Dodoma!
Afisa habari na uhusiano wa Mfuko wa Pensheni (PPF) Edwin Kyungu akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Kidato cha Tatu wa Shule ya Sekondari Wella ya Mjini Dodoma kuhusu huduma mbalimbali za mfuko huo jana mjini Dodoma wakati wa maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayofanyika Kitaifa mkoani Dodoma. Mhadhiri katika Chuo cha Mipango Dodoma Emmanuel Nyankweli akiwaeleza wanafunzi wa Kidato …
Chadema Arusha waitaka Kamati Kuu Taifa kuwatimua madiwani sita Arusha
Na Janeth Mushi, Arusha IKIWA ni siku chache tangu uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Arusha Mjini mkoani hapa kujiuzulu, uongozi wa chama hicho mkoani hapa umeiomba Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza madiwani wake sita katika Wilaya ya Arusha Mjini. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo mjini hapa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani hapa, Samson Mwigamba amesema …
Wizara kuchangia mil 300 ujenzi wa hosteli ya wakulima
Janeth Mushi, Arusha WIZARA ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na wafadhili toka nchini Japan imeahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa hosteli kwa ajili ya kulala wakulima wanaotoka katika wilaya mbalimbali katika Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya maonesho ya wakulima (Nanenane). Hayo yalisemwa juzi mjini hapa na Waziri wa Kilimo Chakula na …
Dar ni kero tupu, petroli, diseli yatoweka na kugeuka lulu
Na Joachim Mushi WAFANYABIASHARA wa usafirishaji na wamiliki wa vyombo vya moto jijini Dar es Salaam leo wameendelea kuhaha wakitafuta nishati za mafuta ya dizeli na petroli huku na kule bila mafanikio. Kero hii ilianza tangu jana baada ya Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati za Maji na Mafuta (EWURA) kutangaza kushusha bei bidhaa za mafuta ya dizeli, petroli …