MUVI yaanza kutoa elimu kwa wakulima Njombe

Na William Macha, Njombe MRADI wa Muunganisho wa Wajasiriamali Vivijini (MUVI) kupitia kitengo chake cha habari umeingia Njombe na kufanikiwa kuzungumza na wajasiriamali wa zao la nyanya na alizeti kutoka mkoani humo. Katika hatua ya kwanza kitengo hicho cha habari kimefanya ziara kwenye vijiji vya Igongolwa, Lyamkena, Ikwete, Kiumba, Itipingi, Ibiki, Mahongole, Kifumbe, Uselule na Imalinyi. Wajasiriamali kutoka katika vijiji …

Naibu Waziri awataka maofisa kilimo ‘kuishi’ vijijini

Na Janeth Mushi, Arusha MAOFISA ugani na kilimo nchini wametakiwa kuhama maeneo ya mjini na kwenda vijijini ili kuwasaidia wakulima na wafugaji mbinu anuai za kilimo cha kisasa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika sekta hiyo muhimu hapa nchini. Kauli hiyo imetolewa katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima na wafugaji, Nane Nane juzi na Naibu Waziri wa Tawala …

Mwanaume aishi na simba wiki 5 banda moja, akisaka ‘noti’

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa banda moja la maonesho ya wanyama wakali akiwemo Simba, Aleksandr Pylyshenko ameamua kujifungia banda moja na Simba kaadhaa anaowamiliki ili kuvutia wateja (watalii) wa wanyama hao kwenye biashara yake. Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki mjini Vasilyevka Kusini Mashariki mwa nchi ya Ukraine, ambapo mmiliki huyo wa mbuga za wanyama hao wakali aliamua kuingia kwenye …

Mgomo wa wauza petroli, dizeli waendelea Dar es Salaam

Na Joachim Mushi MGOMO wa kinyemela kwa wauzaji wa mafuta ya petroli na dizeli umeendelea jana mjini Dar es Salaam, ambapo umezua kero kubwa kwa wamiliki wa vyombo vya moto na wafanyabiashara wa usafirishaji abiria jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mtandao wa dev.kisakuzi.com vituo vingi vya kuuzia mafuta vilikuwa havitoi huduma yoyote kwa visingizio kwamba …

DR. MIGIRO KUZINDUA RIPOTI YA UTAWALA BORA YA APRM

Na Mwandishi Wetu, Dodoma NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Agosti 10, 2011 anatarajia kuzindua ripoti mpya ya Mpango wa Bara la Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania, Rehema Twalib, ripoti hiyo itakayoonesha Hali ya Utawala Bora nchini kwa mujibu wa …