Rais Kikwete, Dk. Bilal wamuaga Jenerali Mayunga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete na Makamu wake Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Mawaziri wastaafu, Joseph Sinde Warioba na Salim Ahmed Sailm, wakiwa katika shughuli ya mazishi kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Mayungi kwenye Viwanja vya Kambi ya Jeshi …

Rais Kikwete amuaga Rais wa Somalia

Rais wa Jamhuri ya Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ameondoka nchini leo, Jumatano, Agosti 10, 2011 mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili ya kikazi katika Tanzania.  Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kiongozi huyo wa Somalia ameagwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na viongozi wengine wa …

Tanzania kutoa msaada wa mahindi kwa Somalia

Tanzania imetangaza kuisaidia Somalia kwa kutoa msaada wa tani 300 za mahindi, ili kuwasaidia kupunguza makali ya ukosefu mkubwa wa chakula unaowakabili kiasi cha wananchi milioni 3.5 wa Jamhuri hiyo Tanzania pia imeahidi kutoa misaada mingine kwa nchi hiyo kwa kadri uwezo wa nchi unavyoruhusu katika kuisaidia Somalia kukabiliana na matatizo makubwa ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiusalama ambayo yamekuwa …

Kikwete ampokea Rais wa Somalia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jana, Jumanne, Agosti 9, 2011, amempokea mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais Kikwete. Ndege iliyomleta Rais wa Somalia, iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mjini …

SIDO IRINGA KUTOA MAFUNZO YA USINDIKAJI

Na William Macha, Iringa SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda nchini (SIDO) mkoni Iringa linatarajia kutoa mafunzo ya usindikaji bora bidhaa za chakula hivi karibuni. Akizungumza ofisini kwake meneja mkuu wa shirika hilo mkoani hapa, Gervase Kashebo amesema mafunzo hayo ya usindikaji wa mchuzi, nyanya mvinyo pamoja na bidhaa nyingine zitokanazo na matunda ya msimu yatawalenga wajasiriamali kutoka mkoani Iringa. Aidha ameongeza …