Dk. Shein awataka wananchi kuwafichua wanaofanya magendo ya karafuu

Na Rajab Mkasaba, Pemba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi Pemba kushirikiana na serikali kupambana na wanaofanya magendo ya karafuu kwani hawana nia njema na serikali wala nchi. Amesema kuwa iwapo mwananchi atauza karafuu zake kwa njia ya magendo ajue kwamba kipato kitakachopatikana hakitomsaidia yeye binafsi wala serikali. Dk. Shein aliyasema …

Washukiwa wa machafuko ya London kufikishwa mahakamani leo

Ni washukiwa wa kwanza kushtakiwa kwa vifo vilivyotokea wakati wa machafuko ya jijini London. Watu jumla ya watano walikufa kwenye machafuko yaliyoanza Jumamosi iliyopita. Mwanamume mmoja pamoja na kijana wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama moja ya Birminghman leo kuhusiana na mauaji ya wanaume watatu waliogongwa na gari wakati walipokuwa wakikilinda kitongoji chao dhidi ya waporaji. Ni washukiwa wa kwanza kufikishwa mbele …

Waziri Ngeleja ‘apona’, bajeti yake yapitishwa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma. HATIMAYE Bunge limepitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini baada ya kuifanyia marekebisho na kuwasilisha mpango wa dharura wa kuondoa tatizo la mgawo wa umeme unaolikabili Taifa kwa sasa. Bajeti hiyo ilipitishwa jana kwa mbinde baada ya wabunge kupongea mpango wa dharura kisha kuichambua kabla ya kuridhia mpango mzima. Aliyekuwa na kazi kubwa jana mjini …

Kikwete: Hakuna Mtanzania ataekufa kwa njaa

Na Mwandishi Maalumu, Shinyanga RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewataka wakuu wa wilaya nchini kwa maeneo yanayoonesha dalili za uhaba wa chakula kutoa taarifa haraka ili ziweze kupatiwa chakula kwani taifa lina chakula cha kutosha, hivyo kuwataka Watanzania wasiwe na hofu. Rais Kikwete amewahakikishia Watanzania kuwa hakuna Mtanzania yoyote ambaye atapoteza maisha kwa njaa kwani Tanzania kwa sasa ina chakula …

MUVI kufunga mashine ya kusindika mhogo kijijini Kilosa

Na Mwandishi Wetu, Mbinga UONGOZI wa Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) umekagua jengo ambalo umepanga kuweka mashine ya usindikaji wa zao la mhogo, wilayani Mbinga itakayotumiwa na kikundi cha MUVI kijiji cha Kilosa. Uongozi huo umefanya kazi hiyo hivi karibuni ulipotembelea kijiji hicho mkoani Ruvuma. Akizungumza katika ziara hiyo, Kaimu Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogovidogo (SIDO) mkoani Ruvuma, …

Rais Kikwete amzika Jenerali Mayunga Shinyanga

Na Mwandishi Maalumu, Shinyanga RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete Agosti 12, 2011 aliongoza mamia ya waombolezaji kumzika Luteni Jenerali Silas Peter Mayunga kwenye makaburi ya Wasabato ya Unyanyembe mjini Maswa mkoani Shinyanga. Jenerali Mayunga, shujaa wa Operesheni Chakaza ya kumung’oa Idi Amin baada ya kuwa ameivamia Tanzania mwaka 1978, alifariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Apollo ya …