Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kanali mstaafu Issa Machibya (katikati) akifungua mafunzo ya wiki moja ya wakufunzi wa Sensa ya majaribio itakayofanyika kuanzia Septemba 4 mwaka huu nchini kote. Wakufunzi hao wanatarajiwa kusambazwa sehemu mbalimbali ili kutoa mafunzo kwa watu watakaoshiriki kuendesha Sensa ya majaribio. Wengine ni – Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu , Dk. Albina Chuwa …
Dk. Bilal akabidhi zawadi kwa washindi mashindano ya Qur-an
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Mariam Salum Mohamed (15) kutoka Tarbiyatul-Islamiyah Pemba, aliyeibuka na jumla ya Pointi 97 katika mashindano hayo yaliyofanyika Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kuliani ni Mufti …
Dk Shein atembelea vituo vya ununuzi karafuu Pemba
Na Rajab Mkasaba, Pemba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameendelea na ziara yake kisiwani Pemba kwa kutembelea vituo vya ununuzi wa karafuu pamoja na kambi za karafuu na kueleza azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kulirejeshea hadhi yake zao la karafuu. Dk. Shein alikuwa akiwaeleza wananchi wakiwemo wamiliki wamiliki wa makambi …
Rais Kikwete atuma rambirambi kwa balozi Nhigula
RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Balozi na Mwanasiasa George Nhigula ambaye aliaga dunia usiku wa kuamkia Agosti 13, 2011 katika Hospitali ya Mikumi, Magomeni, Dar es Salaam kwa matatizo ya figo. Mzee George Maige Nhigula ambaye alizaliwa Aprili 3, mwaka 1929, Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza, ameaga dunia akiwa na umri wa …
Wafanyabiashara Mpanda wasota wakisubiri treni
Mpanda, BAADHI ya wafanyabiashara wa mazao walioweka kambi katika kituo cha Reli cha mjini Mpanda, wakisubiri kusafirisha mazao yao wameingiwa na hofu ya uwezekano wa kuharibika kwa mazao yao na kupata hasara ya mamilioni ya fedha. Wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi jana mjini hapa, wafanyabiashara hao walisema iwapo uongozi wa Shirika la Reli hautachukua hatua za haraka kuwezesha kusafirishwa …
NHC kuondoa nyumba ndogo mijini na kujenga maghorofa
Dodoma, SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) lina mpango wa kuondoa nyumba ndogo katika maeneo yenye thamani kubwa yaliyojengwa holela mijini na badala yake kujenga maghorofa kukidhi mahitaji ya makazi. Taarifa hiyo imetolewa juzi mjini hapa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alipokuwa akimkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuzindua ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Medeli mjini Dodoma. …