kitabu ” UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA LETU” bado kipo mtaani.

    kwa mawasiliano zaidi ya jinsi ya kupata kitabu hiki, piga simu no, 0655025609                                                                                                      0786025609                                                                                          kisandudp@yahoo.com

Hali ya wakili anayedaiwa ‘kutapeli’ mabilioni bado tete, kesi yaendelea

Na Janeth Mushi, Arusha WAKILI maarufu mkoani hapa Mediam Mwale, ambaye juzi alisomewa mashitaka 13 ya kuhujumu uchumi na kughushi nyaraka na kujipatia fedha sh. bilioni 18 kinyume cha sheria bado anaendelea kusota wodini katika hospitali ya Mkoa ya Mt.Meru kwa matibabu kutokana na hali yake kutokuwa nzuri kiafya. Mwale aliyesomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya …

Breaking Newz, Simba wapeleka kilio Jangwani, waikung’uta Yanga 2-0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam HADI pambano la ngao ya hisani kati ya Simba na Yanga linalofanyika katika uwanja wa taifa Dar es Salaam matokeo ni kwamba, Simba inaongoza kwa mabao mawili kwa bila (2-0). Haruna Moshi ndiye wa kwanza kuifungia Simba katika dakika ya 16 huku Felix Sunzu akiongeza goli la pili katika dakika 38. Mpira sasa ni …

Wakili asomewa mashtaka akiwa amelazwa hospitalini

Na Janeth Mushi, Arusha MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, jana amemsomea mashitaka 13 ya uhujumu uchumi wa nchi kwa kughushi nyaraka na kujipatia fedha zaidi ya sh. bilioni 18 Wakili maarufu jijini hapa, Medium Mwale akiwa katika hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru ambako amelazwa kwa matibabu. Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa …

Maofisa wastaafu wa JWTZ waagwa Dar es Salaam

Maafisa wa Jeshi la wananchi wa Tanzania Jeshi la Kujenga Taifa wakiwasukuma gari maalum kwa ajili Mameja Jenerali wastaafu wa Jeshi hilo mara baada ya gwaride rasmi la kuwaaga jana katika Kambi ya Abdallah Twalipo jijini Dar es salaam. Kulia ni Meja Jenerali (mstaafu) Yodan Mtaluma Koyi na Meja Jenerali(mstaafu) Salim Suleiman. Mkuu wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la …

Mkuu wa zamani wa Jeshi Zimbabwe afa kwa moto

MKUU wa zamani wa Jeshi la Zimbabwe amefariki dunia akiwa ndani ya shamba lake, hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi ilizozipata BBC. Taarifa zaidi zinasema Mujuru (62) aliyekuwa mwanasiasa mwandamizi na mume wa Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Bi. Joice Mujuru, inaelezwa kuwa amekufa baada ya kuungua kwa moto uliozuka katika shamba lake lililopo eneo la Beatrice. Ofisa mmoja …