Na Joachim Mushi KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo amepokelewa kama mfalme alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini kurejea kazini baada ya kuchunguzwa na kuonekana hana kosa dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake kutokea bungeni. Jairo aliwasili katika ofisi za wizara hiyo majira ya saa tatu na dakika 16 asubuhi ya leo na kupokelewa …
CCM yasema malalamiko ya Rostam hayainyimi ‘usingizi’ Igunga
Na Joachim Mushi CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema malalamiko aliyoyatoa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz pindi anajiuzulu hayawezi kuwanyima ushindi katika uchaguzi mpya unaotarajiwa kufanyika ili kuziba nafasi hiyo baada yam bunge huyo kujiuzulu. Akizungumza na dev.kisakuzi.com leo katika mahojiano, Katibu Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema chama hicho kina utaratibu maalumu wa …
Kesi dhidi ya Strauss-Kahn yafutwa
JAJI wa Mahakama mjini New York amefuta kesi ya dhuluma za ngono dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani, Dominique Strauss-Kahn. Hatua hiyo imejiri wakati waendesha mashtaka walitilia shaka uaminifu wa mwanamke anayemshtaki, ambaye ni mhudumu wa hoteli moja, Nafissatou Diallo , mwenye umri wa miaka 32. Bw Strauss-Kahn mwenye umri wa miaka 62, alituhumiwa kumshambulia mwanamke huyo, …
Gaddafi: Aluta Kontinua, nitapambana hadi kifo
KANALI Muammar Gaddafi ameapa kupigana na waasi hadi kifo au ushindi, ripoti zimesema, baada ya waasi kudhibiti makazi yake mjini Tripoli. Televisheni inayomuunga mkono Kanali Gaddafi, al-Urubah, imesema Kanali Gaddafi ambaye bado hajulikani alipo, ametoa hotuba akisema kuondoka kutoka kwa makazi yake kulikuwa ni ”mpango”. Makazi hayo ndiyo yaliyokuwa maeneo ya mwisho chini ya udhibiti wa Kanali Gaddafi mjini Tripoli. …
Mambo yageuka Tripoli, waasi warudishwa nyuma na Jeshi la Gaddafi
MAPIGANO yanaendelea kati ya pande mbili muhimu Mji Mkuu wa Libya, Tripoli, kwa siku ya tatu mfululizo huku wapiganaji waasi wakipambana na vikosi vinavyomtii Kanali Muammar Gaddafi. Milio ya risasi na milipuko imekuwa ikisikika karibu na hotel inayotumiwa na vikosi vya serikali pamoja na eneo la makazi ya kiongozi wa Libya ya Bab al-Aziziya. Usiku mzima, mtoto wa Kanali Gaddafi, …
CAG athibitisha Jairo hana atia, Luhanjo amrejesha kazini
Na Joachim Mushi MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesethibitisha tuhuma zilizotolewa Bungeni Julai 18, mwaka huu, dhidi ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo si za kweli na hivyo katibu huyo hana kosa. Taarifa hiyo imetolewa leo Dar es Salaam kwa waandishi wa habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo pamoja …