JK amsimamisha tena Jairo, ni kupisha uchunguzi

Na Mwandishi Wetu RAIS Jakaya Kikwete amemsimamisha tena Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, David Jairo kupisha uchunguzi ambao utafanywa na Kamati Maalumu ya Bunge juu ya tuhuma zinasomkabili kiongozi huyo. Jairo amesimamishwa ikiwa ni siku moja tu baada ya kuanza kazi akitokea mapumzikoni alipokuwa amesimamishwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kupisha uchunguzi uliofanywa na Mdhibiti na …

Ofisa ugavi mahakamani kwa kugushi vyeti vya taaluma

Na Janeth Mushi, Arusha ALIYEKUWA Ofisa Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Elizabeth Kisanga jana amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kwa kosa la kugushi vyeti vya sekondari na vya taaluma ya ugavi, kinyume cha taratibu na sheria. Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya hiyo, Devotha Msofe, Wakili wa Serikali, Sabina Silayo, aliieleza Mahakama kuwa …

Viongozi Chadema wafikishwa mahakamani kwa ujambazi

Na Janeth Mushi, Arusha KATIBU wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Wilaya ya Arusha, Anold Kamdye na aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, Gervas Mgonja, jana wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha. Mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Agustine Kombe alidai kuwa …

Utumishi Zanzibar wamuunga mkono Dk Shein

Na Rajab Mkasaba, Zanzibar WIZARA ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imeahidi kuunga mkono juhudi na bidii anazochukua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika kufanikisha maendeleo ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira bora Watumishi wa Umma na kuimarisha Utawala Bora. Uongozi wa Wizara ya Nchi …

Wajasiriamali Tanga watakiwa kuungana

Na Mwandishi Wetu, Tanga WAJASIRIAMALI mkoani Tanga wametakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) ili kufanikisha lengo la kuunganisha nguvu za wajasiriamali na hatimae kujikwamua na umasikini. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Ndibalema Kisheru katika uzinduzi wa shughuli za wadau wa habari wa mradi wa MUVI mkoani hapa. …

Bunge lamng’ang’ania Jairo, launda tume kumchunguza umpya

Na Mwandishi Wetu, Dodoma SIKU moja baada ya Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo kumrejesha kazini, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo mambo yamegeuka bungeni na sasa bunge limetamka kuunda tume ya kuchunguza zaidi tuhuma dhidi ya Jairo. Alieanza kuonesha hali ya kutoridhika kwa hatua hiyo alikuwa ni Mbunge Kabwe Zitto wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, ambaye leo …