Na Janeth Mushi, Arusha WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Mkuchika ameamuru madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliofukuzwa kuendelea na vikao na kulipwa posho zao hadi mahakama itakapotoa uamuzi juu ya kufukuzwa kwao. Katika barua ya Mkuchika yenye kumbukumbu namba HA.23/235/01/06 iliyotolewa Agosti 23 na kumfikia Mkurugenzi …
Wakili aomba viongozi Chadema waonywe
Na Janeth Mushi, Arusha WAKILI wa Serikali, Edwin Kakolaki ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kutoa onyo kali katika kesi inayowakabili viongozi wa juu wa CHADEMA, hasa kwa washtakiwa wawili yaani mchumba wa Dk. Wilbroad Slaa, Josephine Mshumbuzi na Dadi Igogo kwa kile kutohudhuria mahakamani huku wakiwa na sababu zisizo na msingi. Kakolaki aliomba mahakama kupanga tarehe ya …
Ikulu yatolea maelezo sakata la Jairo
TAARIFA YA UFAFANUZI Tarehe 21 Julai, mwaka huu, 2011, Katibu Mkuu Kiongozi Bwana Phillemon Luhanjo, akitumia madaraka yake ya Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wa Umma, alitangaza hatua ya kumpa likizo ya malipo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishatai na Madini, Bwana David Kitundu Jairo, ili kupisha uchunguzi aliokuwa ameuagiza ufanyike dhidi yake. Bwana Luhanjo alichukua hatua ya kumsimamisha Bw. …
UN yashambuliwa kwa mabomu Nigeria
MWANDISHI wa BBC Bashir Sa’ad Abdullahi ambaye yupo katika eneo la mlipuko amesema ghorofa ya chini ya jengo hilo imeharibika sana. Huduma za dharura zinaondoa miili ya watu kutoka katika jengo hilo huku majeruhi wengine wakipelekwa hospitali, anasema mwandishi wetu. Makundi ya wanamgambo wa Kiislam wamekuwa wakifanya mashambulio katika jiji hilo katika siku za hivi karibuni. Bomu la kutegwa ndani …
Maonesho ya sita ya wajasiriamali wadogo Kanda ya Kusini
MAONESHO ya wajasiriamali wadogo na wakati katika sekta ya Viwanda yanayoratibiwa na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Kanda ya Kusini kufanyika mkoani Ruvuma mwaka 2011. Hayo yamesemwa hivi karibuni na Kaimu Meneja wa SIDO, Mkoa wa Ruvuma Bw. Athur Ndedya. Bw. Ndedya akizungumza na wanahabari alisema “SIDO imekuwa utaratibu wa kuandaa maonesho ya wajasiriamali kikanda kila mwaka. Maonesho haya …
Madaktari: Tiba ya Babu imeleta maafa
Chama cha Madaktari nchini (MAT) kimesema tiba inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila, kwa njia ya kikombe kwa ajili ya kutibu magonjwa sugu, imeleta maafa makubwa kwa wagonjwa. Makamu wa Rais wa MAT, Dk. Primus Saidia, alitoa tamko hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana suala zima la magonjwa yasiyoambukiza …