Na Mwandishi Wetu, Makete WATUMISHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete ambao wanajijua wameambukizwa Ukimwi wameshauriwa kuacha kusambaza ugonjwa huo kwa wengine. Sambamba na mwito huo, wamehimizwa kujitokeza kupima virusi vya Ukimwi kwa hiari mara kwa mara ili kujitambua na kuchukua uamuzi. Ushauri huo umetolewa mjini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Imelda Ishuza wakati akifungua …
‘Ushauri wa Dk. Shein umeongeza ufanisi kwa watendaji’
Na Rajab Mkasaba, Zanzibar OFISI ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi imeeleza kuwa maelekezo na ushauri unaotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa watendaji kila mara, umeongeza ari ya utendaji na ufanisi wa kazi. Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi uliyasema hayo katika kikao …
Kero ya maji ‘yawatibua’ nyongo wana-Ludewa
Na Mwandishi Wetu, Ludewa WANANCHI Ludewa Mjini, mkoani Njombe wamedai hawaoni umuhimu wa kuendelea kuwepo kwa Mamlaka ya Maji Ludewa Mjini (LUDWSSA) kwa sababu inaonekana kushindwa kutoa huduma kwa wananchi. Wakizungumza kwa nyakati na mtandao huu, wananchi hao walisema mamlaka hiyo imeshindwa kuwapatia maji ya uhakika, huku serikali ya wilaya hiyo nayo ikisuasua kuchukua hatua kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi. …
Kilimanjaro walilia sukari, yaadimika kilo sasa 2,500/-
Na Joyce Anael, Moshi WANANCHI mkoani Kilimanjaro wameiomba Serikali kuingilia kati tatizo la mfumuko wa bei ya sukari kutokana bei kupanda ghafla kutoka sh. 1,800 kwa kilo hadi kufikia sh. 2,500 kwa kilo licha ya sukari kuzalishwa kwa wingi katika kiwanda cha sukari cha TPC wilayani Moshi mkoani humo. Wananchi hao wamesema wanashagazwa na ongezeko la bei la ghafla huku …
Ikulu: JK hajababaika kutoa uamuzi suala la Jairo
JULAI 21, 2011, Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, akitumia madaraka yake ya Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wa Umma, alitangaza hatua ya kumpa likizo ya malipo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishatai na Madini, Bwana David Kitundu Jairo, ili kupisha uchunguzi aliokuwa ameuagiza ufanyike dhidi yake. Bwana Luhanjo alichukua hatua ya kumsimamisha Bw. Jairo kufuatia tuhuma zilizokuwa zimeelekezwa dhidi yake …
HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUTOA HOJA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA NNE WA BUNGE TAREHE 26 AGOSTI 2011
Mheshimiwa Spika, 1. Leo tumefikisha Kikao cha 56 tangu tuanze Mkutano wa Nne wa Bunge lako Tukufu tarehe 7 Juni 2011. Mkutano huu ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kujadili Mpango na Bajeti ya Serikali pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Wizara, Mikoa na Taasisi mbalimbali kwa mwaka 2011/2012. Tumejadili masuala mbalimbali na hasa ya kuiletea Nchi …