Swala ya Idd jijini Dar es Salaam leo

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wakiswali swala ya Idd. Waislamu wote leo wameungana na Waislamu ulimwenguni kote kusherehekea Siku Kuu ya Idd baada ya kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. (Picha kwa hisani ya FullShangwe Blog).

Mzee wa miaka 60 ambaka mtoto miaka 4

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamtafuta Daudi Giliama ambaye ni mzee wa umri wa miaka 60 kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka minne (4). Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishina Msaidizi- ACP, Diwani Athumani amesema taarifa zinaeleza tukio hilo limetokea Kijiji cha Igutwa, wilayani Kahama. Alisema mzee …

CCM yampitisha mgombea Igunga, kumnadi kwa helkopta

Na Mwandishi wetu KIKAO cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilichokutana jana jijini Dar es Salaam kimemteua Dk. Dalaly Peter Kafumu kuwa Mgombea wa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Igunga. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, CCM imekubaliana kufanya kampeni …

Ni foleni kila ‘sehemu’ jijini Dar es Salaam

Leo maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam yalikuwa na foleni kama yalivyokutwa na mpigapicha wa dev.kisakuzi.com. Pichani ni foleni barabara ya Morogoro eneo la Magomeni Mapipa. Hii ni foleni maene ya Mtaa wa Msimbazi Kariakoo. Pichani juu ni foleni ya magari eneo la Mnazi Mmoja. Foleni barabara ya Sekilango, Sinza. (Picha zote na Joachim Mushi)

Maandalizi ya Siku Kuu ya Idd ndani ya Jiji la Dar

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakipita katika maduka anuai eneo la Kariakoo kujipatia maitaji mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Idd, ambayo huenda ikawa leo au kesho kulingana na kuandama kwa mwezi (Picha na Joachim Mushi)