Na Mwandishi Wetu, Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed shein amesema jumla ya watu 106 hadi sasa wamethibitika kupoteza maisha baada ya Meli ya abiria na mizigo ya Mv. Spice Islander usiku wa kuamkia Septemba 10, 2011. Wakati Dk. Shein akitoa taarifa hiyo, Rais wa Tanzania, Jakaya Kiwete alipowatembelea majerui jana jioni, ameelezwa …
JK atuma rambirambi vifo vya wananchi katika ajali ya meli Zanzibar
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kuomboleza msiba mkubwa wa vifo vya mamia ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Septemba 10, 2011 …
Ajali ya meli Zanzibar: 163 wahofiwa kufa
WATU wasiopungua 163 wamekufa baada ya meli iliyokuwa imejaa watu na mizigo kuzama katika pwani ya kisiwa cha Unguja. Inadhaniwa kuwa zaidi ya watu 500 walikuwa ndani ya chombo hicho. Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani walipo, lakini watu 325 walionusurika wameokolewa, kwa mujibu wa waziri wa masuala ya dharura wa Zanzibar. Meli hiyo, MV Spice Islander ilikuwa ikisafiri kati …
Breaking News; Ajali juu ya ajali Zanzibar, hadi sasa 250 waokolewa kwenye ajali ya Meli ya Spice
TAARIFA ambazo zimetumwa na mmoja wa mashuda, kutokea Zanzibar, anasema ajali nyingine ya gari imetokea na watu watatu wamekufa papo hapo kati ya wananchi ambao wanaelekea eneo la Nungwi kuangalia ndugu zao waliopata ajali kwenye Meli ya Spice Islanders. Na taarifa za sasa zinaeleza, watu 250 wameokolewa wakiwa hai katika meli iliyozama ya Mv Spice Islanders iliyokuwa ikitokea Bandari ya …
Meli yazama na abiria na mizigo Pemba
TAARIFA ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba, idadi kubwa ya abiria wanahisiwa kupoteza maisha baada ya Meli ya LCT Spice Islanders kuzama katika Bahari ya Hindi, Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba. Akizungumzia ajali hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku ambapo meli hiyo ilikuwa imebeba …
Pingamizi kesi ya madiwani Chadema zasikilizwa
Na Janeth Mushi, Arusha HAKIMU wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Hawa Mguruta amekubali kusikiliza pingamizi la wadaiwa ambao ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe katika kesi iliyofunguliwa na madiwani watano kupinga kufukuzwa uanachama. Aidha pingamizi hizo zilizotolewa kwa njia ya maandishi na wakili upande wa wadaiwa, Method Kimomogolo zinaeleza kuwa Mbowe hawezi kushtakiwa binafsi, CHADEMA haiwezi kushtakiwa …