Na Janeth Mushi, Arusha MWENYEKITI wa Kata ya Lemara iliyopo katika Manispaa ya Arusha, George Madumba (54) amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Rockies iliyopo eneo la Tengeru Wilayani Arumeru mkoani Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi, Leonard Paul alisema kifo hicho kilitokea juzi …
Arusha watakiwa kutenga maeneo ya wazi
Na Janeth Mushi, Arusha UONGOZI wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na idara ya ardhi wametakiwa kutenga maeneo ya huduma za kijamii ikiwemo sekta ya elimu wakati wanapogawa ardhi katika maeneo mapya. Changamoto hiyo imetolewa juzi mjini hapa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye alipokuwa akihudhuria hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya …
SBL kufadhili masomo kwa wanafunzi wasiojiweza 2011
Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imetangaza kuanza kwa mchakato wa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa mwaka 2011. Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 12 kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, Teddy Mapunda. Kwa mujibu wa Bi. Mapunda amefafanua kuwa mpango huo wa ufadhili uko wazi kwa …
Salamu za rambirambi kutoka mtandao wa Hakielimu
Tunatoa pole kwa Watanzania wote kwa msiba uliotakana na ajali ya meli huko Tanzania visiwani. Mwenyezi Mungu awalaze ndugu zetu wote waliotangulia mbele za haki, mahali pema peponi.
Salam za Rambirambi kutoka Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)
WATANZANIA tunaoishi ujerumani tumesikitishwa sana na habari mbaya ya ajali ya meli iliyotokea 10.09.11 katika bahari ya hindi katikati ya visiwa vya Pemba na Unguja nchini Tanzania. Ajali hii ni pigo na msiba mkubwa kwa Taifa letu. Salam za rambirambi ziwafikie Familia za wafiwa, Viongozi wa Tanzania, na watanzania wote kwa ujumla. Umoja wa watanzania ujerumani (UTU) kwa masikitiko makubwa …
Dk. Chami afungua maonesho ya wajasiriamali Mbinga
Na Dunstan Mhilu, Mbinga MAONESHO ya wajasiriamali wadogo na wakati Kanda ya Kusini yamefunguliwa rasimi na Waziri wa Viwanda na Biashhara Dk. Cyril Chami katika viwanja vya CCM wilayani Mbinga. Akizungumza na wajasiriamali hao pamoja na wakazi wa mbinga aliwapongeza kwa ukarimu wao wa kukarimu wageni nakuipongeza SIDO Mkoa wa Ruvuma kwa kufanikisha maonesho hayo. Aidha amewataka wana mbinga na …