Zanzibar MAHARUSI watarajiwa, waliokuwa wakienda kufunga ndoa katika Kisiwa cha Pemba mjini Zanzibar, ni miongoni mwa watu ambao wanasadikiwa kuwa miili yao imenasa katika meli hiyo. Mpaka sasa miili ya watu 240 waliofariki katika ajali hiyo ya meli ya Spice Islender iliyotokea katika eneo la Nungwi, Unguja mwishoni mwa wiki iliyopita, wamepatikana na kuzikwa. Imeelezwa kuwa watarajiwa hao walikuwa wameongozana …
Hizi ndizo faida za kusomesha watoto wa kike
Na HakiElimu JIULIZE, kati ya mwanaume na mwanamke aliyesoma; ni nani huwakumbuka wazazi wake zaidi? Ni nani hajali watoto na familia yake zaidi? Ni nani hurudi kijiji kwao mara kwa mara? Ni nani mwaminifu wa kipato chake? Ni nani hujali afya ya uzazi na malezi zaidi? Majibu ya maswali haya ndiyo sehemu ya mjadala wa leo kuhusu faida za kusomesha …
JK ashiriki dua ya kuwaombea waliokufa ajali ya meli Zanzibar
RAIS wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete leo ameshiriki katika dua ya pamoja kuwaombea marehemu waliofariki dunia katika ajali ya Meli ya Mv. Spice Islanders iliyotokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita. Rais Kikwete katika dua hiyo ameungana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi na wananchi wa Zanzibar. Zifuatazo ni picha kuonesha dua ya pamoja.
Waokoaji kutoka Afrika Kusini wawasili Tanzania
Na Mohammed Mhina, wa Polisi Zanzibar WAPIGAMBIZI 12 toka nchini Afrika ya Kusini, wamewasili usiku wa kuamkia leo mjini Zanzibar kuungana na wazamiaji wengine wa vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini kufanya uhakiki wa kujua kama bado kuna miili iliyonasa kwenye Meli ya Mv. Spice Islander iliyozama chini ya bahari eneo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja usiku wa Jumamosi …
Pinda, Lowassa wawasili Zanzibar kutoa pole kwa Dk. Shein
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu ndogo Migombani na kumpa pole kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya Spice Islanders hapo juzi alfajiri. Waziri Pinda akiwa amefuatana na baadhi ya Mawaziri wa …