WANAUME wawili ambao walishtakiwa kwa kuhusika na ulipuaji wa mabomu mjini Kampala mwaka uliopita wamekiri makosa hayo. Wawili hao ni miongoni mwa washukiwa 14 ambao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo mauaji ya watu 70 katika mashambulio hayo. Washukiwa wa mashambulizi hayo walikuwa 19 lakini watano wakaachiliwa huru jana na Mahakama Kuu mjini Kampala. Wengine miongoni mwao raia wawili wa Tanzania …
Hatma ya madiwani waliofukuzwa Chadema kujulikana!
Na Janeth Mushi, Arusha HATMA ya Madiwani watano waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuendelea na uanachama wao au la itajulikana Septemba 20 mwaka huu. Hatma hiyo itajulikana Septemba 20 baada ya mawakili upande wa wadaiwa, Method Kimomogolo na wakili upande wa wadai Severine Lawena kuwasilisha pingamizi zao mahakamani hapo kwanjia ya maandishi. Hawa Mguruta anayesikiliza kesi …
CCM yawasili Zanzibar kutoa pole ya msiba
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar UONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, umefika Ikulu mjini Zanzibar leo na kumpa mkono wa pole Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander hivi karibuni. Akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa viongozi hao Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania …
MUVI yang’ara Maonesho ya Wajasiriamali
Na Dunstan Mhilu MUUNGANISHO wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) umefanikiwa kufanya vizuri katika Maonesho ya wajasiriamali wadogo na wakati Kanda ya Kusini yaliyokuwa yakifanyika hivi karibuni wilayani Mbinga, kwenye viwanja vya CCM. Banda la MUVI lilionekana kusheheni kila aina ya vipeperushi vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili yakutoa elimu kwa wajasiriamali hususani wa zao la muhogo na alizeti waishio Mkoa wa Ruvuma. Vipeperushi …
Tanzania isikubali misaada yenye masharti magumu-Wanaharakati
Na Joyce Ngowi MWANAHARAKATI wa Kimataifa kutoka nchini Ghana, Profesa Dzodzi Tsikata ameishauri Serikali ya Tanzania kuacha utegemezi wa misaada midogo yenye masharti magumu na badala yake kuangalia namna nzuri ya kutatua matatizo ya raia wake kwa manufaa ya Taifa zima. Prof. Tsikata ametoa changamoto hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) alipokuwa …