“How To Pass Any Exam without Fear!”

Attention Parents… “Amazing, new book reveals… “How To Pass Any Exam without Fear!” IF you are interested in helping your child to Pass Exams without Fear this year, and get better grades quickly and easily then this is going to be the most exciting message you’ll ever read! Here’s why: There is an amazing new book called, ‘Winning the battle- …

Rais wa Comoro kuwasili leo Tanzania

Na Mwandishi Maalumu RAIS wa Comoro Dk. Ikililou Dhoinine anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo Septemba 15, 2011 kufanya ziara ya kikazi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu Dk. Dhoinine atawasili majira ya mchana na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. …

Wazamiaji wa Afrika Kusini ‘wachemsha’ washindwa kuifikia meli, waomba msaada

Waagiza Sub Marine kutoa Afrika Kusini Na Mwandishi Wetu, Zanzibar KAZI ya kuopoa miili ya watu walionasa kwenye mabaki ya Meli ya Mv. Spice Islanders lililokuwa likifanywa kwa pamoja na wazamiaji kutoka nchini Afrika ya Kusini na Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania hatimaye imeshindikana. Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu imezipata leo toka kwa Ofisa Habari wa Jeshi …

Ndege yaanguka Angola yaua Majenerali

AJALI ya ndege nchini Angola imesababisha vifo vya watu 26, wakiwemo majenerali wa kijeshi watatu, Ofisa wa Serikali ameiambia BBC. Luis Caetano, Msemaji wa Mamlaka ya Jimbo la Huambo, amesema ndege hiyo ya kijeshi ilianguka baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Huambo. Amesema watu sita wameokoka kwenye ajali hiyo, akiwemo rubani na msaidizi wake. Waandishi wa habari wamesema …

Basi lapinduka lauwa 10 na kujeruhi 19

BASI la abiria aina ya Scania lenye namba za usajili T 591 ABK (Brazila) limepata ajali leo eneo la Mwida, Ubena kilomita kadhaa ukitokea Morogoro ambapo watu 10 wamepoteza maisha. Akizungumzia ajali hiyo kutoka eneo la tukio Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Sarehe Mbaga amesema kati ya watu waliokufa wanawake ni 7 na wanaume watatu (3). …

KCB yatoa msaada wa vifaa vya hospitali

Na Mwandishi Wetu, Mwanza BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo vya tiba kwa hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, iliyopo Butimba ya jijini Mwanza ili kusaidia akinamama wanaojifungua. Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 4,9/- vilikabidhiwa kwa uongozi wa hospitali hiyo na Meneja wa tawi la Mwanza, Walter Lema na kupokekelewa na Mganga Mkuu Mfawidhi wa …