Ongezeko la ajali barabarani zamkera Waziri

*Abuni njia mpya kudhibiti ajali Na Joachim Mushi ONGEZEKO la ajali za barabarani zimemkera Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha na sasa amependekeza utaratibu mpya ambao unaweza kudhibiti matukio mengi ya ajali hizo. Waziri Nahodha ambaye ndiye mwenye mamlaka ya usimamizi wa sheria barabarani kupitia Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, amepende sasa kuanza utaratibu …

Mwenyekiti wa Wilaya Chadema ahamia CCM

Na Bashir Nkoromo, Singida KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameshushia kilio tena kwa CHADEMA baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Singida Mjini, Nakamia John kukamia CCM. Nakamia ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, alitangaza kuhamia CCM na kukabidhi kadi yake ya CHADEMA …

SBL yazindua kampeni ya unywaji wa pombe kistarabu

*Kutoa elimu nchi nzima kuwalinda raia Na Joachim Mushi WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha ameipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), kwa kuzindua kampeni ya kupinga unywaji wa pombe kupindukia wa pombe ambao umekuwa na madhara mengi kwa muhusika na Taifa kwa ujumla. Nahodha ametoa pongezi hizo leo alipokuwa akizindua rasmi kuanza kwa kampeni hizo …

Serikali yasitisha kazi ya kutafuta maiti majini

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetoa tamko la kusitishwa rasmi shughuli ya utafutaji wa miili ya watu walionasa kwenye meli ya Mv. Spice Islanders iliyozama eneo la Nungwi Kaskazini mwa Kisiwa cha Unguja, Zanzibar kutokana na ugumu wa utekelezaji wa kazi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar, …

Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika ndani ya TGNP

Usiku huu Septemba 15, 2011 ndani ya Viwanja vya TGNP linaendelea Tamasha la Kumi la Jinsia, wanaharakati wanaoshiriki Tamasha hilo wanakutana kwa pamoja kwenye hafla ya Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika. Hapa kuna burudani na shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanaharakati kienzi utamanduni wa Mwafrika. Zifuatazo ni picha mbalimbali ndani ya hafla hiyo;

Rais Kikwete amtumia rambirambi RC wa Pwani

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Hajat Amina Mrisho kufuatia vifo vya watu 10 na wengine 19 kujeruhiwa kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea Septemba 14, 2011 katika kijiji cha Mwindu wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani. Ajali hiyo ilitokea baada ya basi la Kampuni ya Grazia Safari’s kupinduka likitokea Songea …