Care International Tanzania Yawakutanisha Wadau wa Taasisi za Kifedha

Mkurugenzi mwendeshaji kutoka Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Fedha (FSDT) Bi. Irene Madeje Mlola akitoa maelezo jinsi wanavyofanya jitihada kupanua wigo kwa watu mbalimbali wenye mahitaji ya huduma za kifedha.

 

Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dkt Ashatu Kijaji akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa tatu wa kitaifa juu ya huduma za Kifedha kwa vikundi vya hisa, mjadala wa masuala ya kisera na kisheria katika uhusishwaji wa kifedha ulioandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Care International Tanzania, Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Care International nchini Tanzania Bw. Paul Daniel akiwa anatoa maneno ya utangulizi na kuwaeleza wadau malengo ya mkutano huo pamoja na shirika la Care kwa wadau waliohudhuria katika mkutano huo.
 Muwezeshaji katika mkutano huo ambaye ni Mkurugenzi wa Programu ya (GEWE) Bi. Mwanahamisi Sigano akitoa mwongozo wakati wa mkutano huo.
 
 Mwalimu Debora kutoka Kibaha ambaye ni mjasiliamali na mmiliki wa vikundi mbalimbali vya kijasiliamali akieleza namna Asasi ya Kiraia ya Care International Tanzania ilivyo msaada kwao pamoja na Taasisi za kibenki kwa kuwawezesha kuendelea kiuchumi.
 Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Tanzania Postal Bank (TPB) Bw. Deo Kwiyakwa akielezea Sera na Sheria jinsi zinavyokwamisha katika maendeleo ya taasisi za kifedha.
Bi. Zenais Matemu ambaye ni Mratibu wa Programu ya Mradi wa Pesa kwa wote akichangia wakati wa mkutano huo ambapo alisema Forum hii ni muhimu na ikiwezekana ikae ili ijadili ni jinsi gani wanavyoweza kusaidia vikundi hivyo ili vipate kuendelea zaidi.
 Baadhi ya wabia kutoka Serikalini na Taasisi binafsi wakichangia mambo mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Wawakilishi wa Serikari  kutoka Wizara ya Fedha, Benki kuu ya Tanzania, TAMISEMI na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) wakijadili swala zima Sera katika uhisishwaji wa kifedha.
 Baadhi ya wawakilishi mbalimbali kutoka katika Taasisi za Kifedha waliofika katika Mkutano huo wakitoa maoni mbalimbali.
Baadhi ya watu mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
Picha na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa Tanzania
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji  amesema kwamba Mfumo jumuishi wa kifedha ni muhimu katika kijenga  uchumi wa taifa la Tanzania. Aliyasema hayo wakati wa mkutano wa tatu wa kitaifa juu ya huduma rasmi za kifedha kwa vikundi vya hisa na mjadala wa masuala ya kisera na Sheria katika uhusishwaji wa kifedha,
mkutano ulio andaliwa na asasi ya kiraia ya Care international ya Nchini Tanzania.
Alisema kuwa ili kuhakikisha swala hili linafanyiwa kazi Serikali imeandaa sera ya mwaka 2006 inayohakikisha mifumo isiyo rasmi ya kifedha inaweza  kuwa rasmi na watu wote wanakuwa wamejumuishwa katika mfumo sahihi wa matumizi  ndani ya sekta ya kifedha.

 

Dkt. Ashatu aliongeza kuwa moja ya changamoto  iliyo katika mfumo usio rasmi wa kifedha ni kukopeshwa kwa riba kubwa na watu wanaofanyakazi katika mifumo hiyo lakini hawajarasmishwa rasmi ambapo inawaumiza wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla na kutokana na hilo Serikali sasa inaandaa sheria kwa ajili ya huduma ndogo za kifedha ilikuwekea mazingira rafiki ya kufanya kazi zao. 
Pia aliongeza kuwa Care international amekuwa mdau mkubwa katika maendeleo ya uchumi nchini Tanzania sio kifedha tu lakini pia sekta ya afya, Kilimo na maeneo mbalimbali aliwasihi wananchi waendelee kuwapa ushirikiano ili kuleta maendeleo zaidi nchini.
Nae Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia Care International Nchini Tanzania Bw. Paul Daniel alisema kuwa lengo la mkutano huo ni muendelezo wa utamaduni wa Care kutoa Fulsa ya kupeana taarifa kwa wadau walio ndani ya sekta ikiwa lengo kubwa ni kuongeza umoja na ushirikiano
katika kuhamasisha uhusishwaji wa kifedha katika vikundi vya Hisa.
Mkutano huu ulihusisha wadau mbalimbali wa Serikali wakiwemo Wizara ya Fedha  na Mipango, Benki kuu ya Tanzania, TAMISEMI na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) pia Taasisi za
kifedha na Sekta mbalimbali, ikiwa ni juhudi za Care nchini Tanzania ambazo zimelenga katika kutoa Fursa kwa jamii kuhamasisha usawa wa kijinsia kwa ubia wakiwahusisha sekta binafsi, Serikali,wabia wa wa maendeleo na asasi za Kiraia (CSO’s).