Wazirii Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais Sakaorzy wa Ufaransa tayari wamewasili nchini Libya kufanya ziara yao.
Viongozi hao wawili ndio wa kwanza kutoka nchi za magharibi, kufika Libya tangu Kanali Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani.
Nchi hizo mbili ambazo ni wanachama wa shirika la kujihami la Nato ziliongoza operesheni za Nato kukabiliana na vikosi vya Kanali Gaddafi.
Wakuu hao wawili walikutana na viongozi kutoka Baraza la Kitaifa la Mpito (National Transitional Justice) mjini Tripoli, na wanatarajiwa kufika hadi Benghazi ngome ya waasi, ambapo wanatarajiwa kutoa hutuba katika uwanja wa Liberty Square. Mkuu wa NTC Mustafa Abdul Jalil amewapongeza wakuu hao kuchukuwa msimamo thabiti wakati wa maasi nchini Libya.
Bw Abdul Jalil, Jumatano, alitoa wito wa usaidizi wa silaha ili NTC iendeleze shughuli za kudhibiti maeneo ambayo bado yanashikiliwa na Kanali Gaddafi, akiongeza kuwa yuko mafichoni kusini mwa nchi hiyo akiandaa namna ya kulipiza kisasi.
Cameron na Sakorzy waliipokea kauli ya Bw Jalil na kuusifu ushupavu wa raia wa Libya, pamoja na kuahidi kuwa wataendelea kuiunga mkono NTC katika lengo lake la kuleta amani na demokrasia.
“Kuna msongomanao wa magari barabarani, kuna maji na hospitali zinatoa huduma , hii inaridhisha” Bw Cameron alisema. “Lakini Gaddafi bado yuko mafichoni. Ni lazima tuendelee na kazi ya NATO kwa manufaa ya usalama wa raia na kukamilisha kazi tulioianza” aliongeza.
“Tutawasaidia kumtafuta Gaddafi na kumshtaki, pamoja na kuwasaida kuziondoa silaha za maangamizi-kama makombora- nje ya nchi.
Sakorzy amewasihi raia wa Libya waepukane na kulipiza kisasi na akatoa wito wa kudumisha umoja pamoja na maridhiano.
-BBC