Bwana Harusi wa Mbunge Atoroka na Michango ya Harusi

Bwana Harusi wa Mbunge Atoroka na Michango ya Harusi

Bwana Harusi wa Mbunge Atoroka na Michango ya Harusi

STAA wa Bongo Fleva na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) anayewakilisha Vijana Mkoa wa Geita, Vicky Pascal Kamata akiwa na mchumba wake Charles Pai. 

Kwamba ile harusi ya the Century iliyokuwa ifanyike leo Kempisk Hotel baina ya Mbunge Maarufu wa Viti Maalum CCM, Vicky Kamata imepiga mwamba kutokana na ukweli kujulikana dakika ya mwisho jana kwamba Mchumba wake Mbunge ni Tapeli wa ajabu hapa nchini amabae amekuwa akiwadanganya sana kina dada wenye utajiri na kwamba, Vicky Kamata anakuwa ni Mbebez wa tatu kutapeliwa na Mchumba huyu pichani. 

Ripoti inasema kwamba siku chache kabla ya siku ya harusi, mke wa kweli wa Mchumba huyo alijitokeza na hati zake Kanisani Catholic kwa Wachungaji waliomfahamisha Mchumba kwamba hakutakuwa na tendo la kufunga Ndoa Kanisani ndipo Mchumba huyo bwana Charles akatimka na jumla ya pesa za mchango wa harusi hiyo shilingi milioni 40.

Jumla zilikuwa zimeshachangwa shilingi milioni 100, tayari USD $ 15,000 zilikuwa zimeshalipiwa kwa ajili ya Ukumbi wa Kempisk Hotel, tayari wageni waalikwa toka Geita walioshiriki kumchagua Mbunge huyo walishafika Dar wapo hapa, na cha kutisha zaidi ni kwamba Mbunge toka jana asubuhi ameshindwa kabisa kumpata mchumba huyo kwenye simu zake zote zimezimwa hazipatikani kabisa.

Inasemekana baadhi ya Wabunge waliomchangia kwa kiwango kikubwa sana wameanza kulalamika kwa pembeni.
-Global Publishers